Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ikiwezekana Kaa Mbali Kabisa Na Watu Hawa

Kuna watu ambao kila ukienda kwao na wazo la kufanya kitu cha tofauti, hata kabla hawajakusikiliza unapanga utafanyaje, tayari wanakuwa na jibu kwamba haiwezekani.

Kaa mbali na watu ambao wanakuambia haiwezekani. Watu wa haiwezekani hawana maana kwenye hii dunia zaidi ya kuwaaminisha wengine kwamba mambo hayawezekani kumbe yanawezekana.

Watu wa haiwezekani, ni watu ambao unapaswa kuwaepuka sana hata kama ni wa karibu kwako.

Watu ambao kila kitu kwao hakiwezekani, kadiri unavyokaa nao wanakuaminisha na kukubadilisha mwishowe unakuja kukubaliana nao kwamba haiwezekani.

Ni bora uamini inawezekana kwa sababu kuamini haiwezekani ni kupoteza nguvu na muda kwa wakati mmoja.

Hatua ya kuchukua leo; waepuke mara moja watu wa haiwezekani kwenye maisha yako. Huku ukiendelea kubaki kwenye mchakato sahihi wa kuweka kazi kuhakikisha unapata kweli kile ambacho wewe unakitaka.

Na wala usijidanganye kwamba utaweza kushirikiana nao kwenye baadhi ya mambo ambayo yanawezekana, ukisharuhusu kuwasikiliza, ukishakaa karibu nao jua kila kitu hakitawezekana kwako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: