Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Yawe Malengo Yako Ya Kwanza Ya Fedha

Chochote ambacho kinatokea sasa kwenye eneo lako la fedha, ni matokeo ya tabia ambazo umejijengea.

Hakuna kinachotokea kama ajali, huwezi kupanda mahindi ukavuna mbaazi. Kila kinachotokea umekisababisha kutokea.

Ni kawaida ya watu, wakishakuwa na fedha zinakuwa zinawawasha wanahakikisha kwanza wazitumie ndiyo wajisikie.

Ndiyo maana watu wakiwa na hela ni rahisi kutapeliwa au kutumia hovyo kwa sababu wanaonesha dalili ya kuwa hivyo.

Sasa akili ya kwanza ya fedha (mentality) ni kutokuitumia.

Ndiyo malengo yako ya kwanza baada ya kupata fedha ni kutokuitumia fedha uliyopata.

Ukipata fedha usishawishike kwenda kuitumia, bali usiitumie.

Ukishajua una matumizi mabaya ya fedha jifanye umefilisika(kuwa broke). Yaani usitembee na fedha kwa ajili kuepuka kununua vitu hovyo bila kuwa na bajeti.

Kutafuta uhuru wa kifedha ni kazi ngumu. Hivyo huwezi kufanikiwa bila kubadili tabia zako zinazokufanya ushindwe kwenye safari yako ya mafanikio.

Hatua ya kuchukua leo; ukipata fedha, hatua ya kwanza usiitumie endelea na maisha yako kama ya mwanzo.

Epuka kufanya matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye eneo la fedha.

Kuwa mbahili, fanya uwekezaji, weka akiba, ongeza kipato, punguza matumizi na utaiona hela.

Fedha ni jawabu la mambo yote kadiri ya kitabu cha mhubiri lakini usipoitumia vizuri fedha itakusaidia kununua matatizo mengi yasiyokuwa na ulazima kwako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: