Design a site like this with WordPress.com
Get started

Changamoto Ya Kukosa Hela Inaanzia Hapa

Ukiona huingizi hela kwenye maisha yako basi changamoto yako ni moja huna unachouza au unauza kidogo.

Fedha inapatikana kwa kutoa thamani kubwa kwa wengine na katika kutoa thamani ndiyo tunapata fedha.

Kifupi fedha ni mbadilishano wa thamani.

Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi.

Ukiweza kuuza zaidi utaweza kutatua changamoto zako zote za kifedha.

Ukilalamika huna fedha jiulize leo umeuza nini? Kama huuzi, tafuta wateja uza, tafuta watu ambao wanahitaji kile unachouza na wauzie.

Kadiri unavyouza zaidi ndivyo unavyopokea zaidi.

Kwenye biashara, mauzo yakiwa makubwa na faida pia inakuwa kubwa. Mauzo ndiyo moyo wa biashara hivyo ili biashara yako au maisha yako yaende yanahitaji fedha kwa sababu fedha ndiyo jawabu la mambo yote kwenye maisha na kwenye biashara.

Hudumia watu wengi na utaweza kuuza zaidi. Kuwa na wateja wengi, changamoto ya mauzo kidogo ni kwamba unahudumia watu wachache hivyo kuwa na wateja wengi na utaweza kuongeza mauzo, ukiwa na wateja wachache ni ngumu kukamilisha mauzo makubwa.

Hatua ya kuchukua leo; Kama hupati fedha zaidi unapaswa kuuza zaidi.

Jitahidi sana kujisukuma kwenye namba ya mauzo. Kadiri unavyouza zaidi ndivyo unavyofanikiwa zaidi.
Kila siku kuwa na malengo makubwa ya mauzo.
Jisukume kuuza zaidi na utapata zaidi.
Kila siku jiambie kwamba wewe ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo unakwenda kukamilisha kiasi fulani cha mauzo na unakitaja kiasi hicho.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: