Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukitaka Watu WasikupuuzeKuwa Hivi

Kuwa bora kiasi kwamba hakuna anayeweza kukupuuza kwenye kile unachofanya.

Hakuna mtu ambaye anafanya vitu vyake kwa ubora halafu watu wakampuuza. Ukishakuwa bora watu watakuheshimu wao wenyewe yaani kifupi, ubora wako utakuheshimisha.

Chochote kinachopita mkononi mwako kifanye kwa ubora wa hali ya juu.

Kama unafanya kazi, ifanye kazi yako kwa ubora kiasi kwamba hakuna atakayekupuuza kwenye kazi yako.

Kama unafanya biashara, hakikisha unatoa huduma bora kiasi kwamba wateja watajisikia vizuri na kunufaika na huduma yako.

Ukifanya vitu vyako kwa mazoea, bila kuweka ubunifu na kujitofautisha na wengine utaendelea kupata matokeo ya kawaida lakini pia watu watakupuuza na kukuchukulia poa.

Usikubali watu wakuchukulie poa, kuwa bora kwa sababu ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Kama wengine wanafanya vizuri sana kwa nini na wewe usifanye vizuri?

Hatua ya kuchukua leo; kuwa bora kwenye kile unachofanya, kazi yako iwe msemaji wako mkuu.

Habari njema ni kwamba kuwa bora ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako, hivyo basi nenda kafanye kazi yako kwa ubora, jali maslahi ya wengine, toa thamani kubwa kwa wengine na wasaidie watu wengi kupata kile unachotaka na wewe utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.

Kumbuka kila unachotoa kwa dunia, asili itakulipa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: