Maisha yetu ni mauzo na kila siku tuko katika mchakato wa mauzo.
Mauzo ndiyo habari ya mjini kwa kila binadamu, kwa sababu mauzo ndiyo yanatufanya tuweze kupata kitu ambacho tulikuwa hatuna.
Kila anayeuza kuna thamani anaitoa kwa mtu mwingine na mtu anapotoa thamani kwa wengine anapaswa kulipwa.
Kumbe basi, hakuna mtu ambaye anatengeneza bidhaa kwa lengo la kuingalia tu, bali tunatengeneza bidhaa kwa lengo la kuuza yaani kuwasaidia wengine kuwa bora.
Tunategemea mauzo sana kwenye maisha yetu kwa sababu mauzo ndiyo njia kuu ya kuleta fedha mifukoni kwetu.
Ikiwa basi wewe ni muuzaji basi kazi yako kubwa katika mauzo ni kuwasaidia watu kufanya maamuzi ambayo ni maamuzi sahihi.
Wateja wengi hawajui kile wanachotaka, kwa sababu wewe ni muuzaji unajua na unauelewa na kile unachouza hivyo ni njia nzuri kwako kuweza kumsaidia mteja wako kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na kile unachouza.
Wewe muuzaji unakuwa na bidhaa na ndiyo unakuwa na uelewa mkubwa sana juu ya kile unachouza hivyo kazi yako kubwa ni kumsaidia mteja kufanya maamuzi sahihi.
Lakini utashangaa baadhi ya wauzaji hawako pale kwa lengo la kumsaidia mteja bali wako pale kwa lengo la kupiga hela, yaani yeye bora auze lakini siyo kumsaidia mteja kupata kitu kizuri na kutatua shida yake.
Unapokuwa na mteja, msikilize kwa makini na kaa kimya wala usimkatishe wakati anaongea.
Wateja wengi wanakuwa na shida ila wanakosa watu wa kuwasikiliza na kutoa ya moyoni.
Hatua ya kuchukua leo; hakikisha unafanya kazi yako katika mauzo ya kumsaidia mteja kufanya maamuzi sahihi ili aweze kupata kile anachotaka.
Mwisho, maisha ni mauzo hivyo hakikisha unakuwa muuzaji bora sana kwenye kile ulichochagua kufanya. Kupitia kile unachouza kiende kuwasaidia watu kuwa na maisha bora.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog