Ni mrejesho.
Siku hizi watu wamekuwa bize kiasi kwamba hata ukiwatumia ujumbe wanashindwa kujibu.
Ukiwatumia watu ujumbe wa meseji za kawaida ndiyo hawajibu kabisa angalau kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kujenga mahusiano imara hii siyo kitu kizuri. Kwa kuwa mawasiliano ni mrejesho, pale mtu anapokutumia ujumbe au kupokea kitu unapaswa kutoa mrejesho.
Kama mtu alitumia muda wake kukupigia, kukutumia ujumbe halafu hutoi mrejesho badala yake unaupuuzia inakuwa siyo kitu kizuri katika mahusiano.
Watu huwa wanakwazika kwa vitu vidogo tu ambavyo wewe unachukulia poa lakini mwenzako kaviweka moyoni.
Malalamiko haya yamekuwa mengi na usipokuwa makini katika mawasiliano utapoteza mahusiano yako.
Kitu cha ajabu ni kwamba, ukimtumia mtu meseji ya kawaida haoni lakini ukimtumia fedha meseji ya tigo pesa au mpesa anaiona.
Katika mawasiliano yoyote yale mrejesho ni zawadi.
Mpe mtu mrejesho kwa kila mawasiliano ambayo anawasiliana na wewe. Usipuuzie ujumbe wowote unaopokea kutoka kwa mtu.
Kwa kitendo tu cha kumjibu ni kuonesha hali ya kujali na kuthamimi muda wake.
Hata uwe bize kiasi gani kuna muda utapata wa kupitia mawasiliano yako kwenye simu na kutoa mrejesho kwa wale watu wote ambao walikupigia au walikutumia ujumbe.
Hatua ya kuchukua leo; Thamini rasilimali za yule anayewasiliana na wewe kwa kumpa mrejesho.
Pata picha umewakwaza watu wengi kiasi gani kwa tabia ya kutokutoa mrejesho baada ya kupigiwa simu na kutokupokea na kushindwa kumtafuta tena au unatumiwa ujumbe halafu hujibu.
Vitu ambavyo unaweza kuvibadili, vibadilli, kumbuka mahusiano mengi yanaendeshwa kwa hisia hata kama wewe hujali jua una haribu mahusiano yako na watu wengine.
Kumbuka mawasiliano ndiyo njia kuu ya kutusaidia sisi kupata kile tunachotaka kutoka kwa wengine. Hivyo usidharau mawasiliano na zawadi kubwa ya mawasiliano ni mrejesho na siyo kupuuzia.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog