Kama tunavyojua mteja ndiyo mfalme kwenye biashara yoyote ile.
Siyo tu ni mfalme bali pia mteja ndiyo bosi. Mteja anaweza kukufukuza kazi hata kama biashara ni yako. Unaweza kujiuliza biashara ni yangu iweje mteja anifukuze? Akiacha kununua kwako na akiwaambia na mwenzake mpaka hapo anakuwa ameshakuharibia biashara yako.
Na unapaswa kujua kwamba, mteja huwa hakosei yuko sahihi mara zote, unapaswa kumsikiliza hata kama anachoongea hakina maana.
Unapokuwa na bidhaa yako unapaswa kuelezea vitu hivi viwili kwa mteja wako.
Moja, elezea manufaa ya bidhaa kwa mteja wako. Ukiwa unamjua mteja wako unapaswa kumuelezea namna bidhaa yako itakavyokwenda kumnufaisha na siyo sifa za bidhaa.
Ukimueleza mteja manufaa anayokwenda kuyapata kupitia huduma yako itamfanya ajisikie vizuri, lengo la kuuza kitu ni kumfanya mteja anufaike na kile unachomuuzia.
Lakini, kama mteja humjui usimwelezee manufaa badala yake mueleze sifa ya bidhaa yako.
Ukikutana na mteja mara ya kwanza mweleze kwanza sifa ya bidhaa yako baada ya kujuana sasa, mwambie manufaa atakayokwenda kuyapata.
Hatua ya kuchukua leo;
Elezea manufaa ya bidhaa yako kwa mteja zaidi kuliko sifa.
Ukiwa humjui mteja wako muelezee sifa ya bidhaa lakini kama unamjua mteja muelezee manufaa atakayokwenda kupata akitumia bidhaa yako.
Bidhaa unayouza ikawe msaada kwenye maisha ya watu na kumnufaisha mteja zaidi baada ya kumtatulia shida yake.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog