Design a site like this with WordPress.com
Get started

Vitu Viwili Pekee Muhimu Kwenye Biashara

Kuna vitu viwili muhimu kwenye biashara sina uhakika kama itakufaa lakini ukivijua vitakusaidia kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara yako.

Moja ni jinsi gani ya kupata wateja. Biashara yako haiwezi kupata wateja kama hujaifanyia masoko.

Masoko ni kuifanya biashara yako ijulikane, kama hujawaambia watu unauza nini watu siyo malaika kuweza kubashiri kile unachouza.

Pambana sana ili uweze kutafuta wateja wapya kwenye biashara yako, ukiwa na wateja wengi itakusaidia kuongeza mauzo na kipato chako kitakuwa yaani faida itaongezeka.

Usijinyime faida kwa kuwa na wateja wachache, tanua wigo wa kuwa na wateja wengi ili kupata mauzo zaidi.

Kitu cha pili ni kutengeneza fedha. Unatengenezaje fedha ? Baada ya kupata wateja yaani baada ya kufanya masoko kazi yako kubwa sasa ni kufanya mauzo.

Hata uwe na bidhaa nzuri kiasi gani kama watu hawaijui na huuzi hapo huna biashara.

Kwenye biashara yako, ustaarabu pekee ni kuuza na siyo kitu kingine. Huwezi kutengeneza fedha kama huna mauzo unayofanya.

Fanya uwezavyo hakikisha ukipata mteja basi unamshawishi kununua kile unachouza. Maana usipouza utashindwa kujiendesha kibiashara.

Mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara yako, inakusaidia kupata fedha zaidi na biashara kwenda vizuri.

Hatua ya kuchukua leo; jisumbue kupata wateja kwa kufanya masoko na tengeneza fedha kwa kufanya mauzo zaidi.

Kwahiyo, kama huuzi au hufanyi masoko usitegemee kufanikiwa kwenye biashara yako.
Sumbuka na masoko na mauzo na nje ya hapo ni kelele na usumbufu.

Kifupi, usisumbuke na mambo ambayo hayakupeleki kwenye mauzo na masoko.
Jitahidi kutoa thamani kubwa zaidi kwenye kile unachofanya lakini pia kutoa huduma bora ambayo inakwenda kutibu maumivu ya mteja wako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: