Ni kawaida watu wakifanikiwa kidogo, mafanikio madogo huwa ni kikwazo kwao.
Kamwe usiridhike na kupata mafanikio kidogo, badala unapaswa kujiweka kwenye hatari mara zote.
Watu waliofanikiwa kidogo, wanakuwa wanaridhika mapema na mafanikio waliyopata na kuendelea kuyalinda.
Badala ya kukazana wafanikiwe zaidi, wao wanakazana kuyalinda zaidi.
Kwa mfano, timu ya mpira inapopata goli moja na kuendelea kulilinda goli hilo na kuacha kushambulia wanajikuta wanashindwa vibaya.
Kwenye maisha, kuwa na machaguo haya mawili.
Moja, jilinde kwa chochote kile ulichonacho, ili kisipotee
Mbili, endelea kushambulia. Usiridhike na kile ulichonacho, kuwa na juhudi zaidi ya kutaka kupata zaidi. Kama ulipata moja, usiridhike na moja bali endelea kutafuta matokeo zaidi.
Kwa mfano, Kama unafanya biashara, usiridhike na mauzo unayopata, badala yake pambana kupata mauzo zaidi.
Usiridhike kuhudumia wateja wale wale kila siku, pambana kutafuta wateja wapya.
Hatua ya kuchukua leo; Jilinde na endelea kushambulia ili upate matokeo mazuri zaidi.
Usiridhike na mafanikio madogo, yatumie kukupa hamasa, yalinde lakini endelea kushambulia mpaka upate matokeo bora zaidi.
Jisukume kila siku kupata kile ambacho hujawahi kupata kwenye maisha yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog