Design a site like this with WordPress.com
Get started

Chochote Unachokisema Vibaya Kinakukimbia

Ukiisema fedha vibaya, itakukimbia.

Na mara nyingi, watu wasiokuwa na fedha, ndiyo wanaongoza kwa kusema vibaya kuhusu fedha.

Iko hivi hivi, chochote ambacho unakisema vibaya kinakukimbia, pata picha umeshavisema vibaya vitu vingapi?

Kama ulishawahi kuisema fedha na matajiri vibaya ilishawahi kukusaidia kupata fedha zaidi? Badala yake? Inakufanya uzikose zaidi.

Watu wasiokuwa na fedha ndiyo wanaongoza kwa kuisema fedha vibaya.

Na ubaya wa fedha unaanza pale usipokuwa nazo. Kwa sababu utakua unahitaji sana kufanya baadhi ya vitu, lakini fedha huna.

Unaweza kupata hasira kwa kuona kwamba wale wenye fedha ndiyo wanakuzuia wewe usipate fedha.

Kifupi tu rafiki yangu, hakuna anayekuzuia wewe kupata fedha zaidi, ni mawazo yako mwenyewe uliyonayo juu ya fedha na wale wenye fedha.

Usiwachukie wale ambao wanafedha wala usiiseme fedha vibaya.

Hatua ya kuchukua leo; ipende fedha na wapende wenye fedha.

Anza kutoa thamani kubwa kwa wengine.

Usiwe na hasira na yeyote bali chukua hatua kuhakikisha unatengeneza kipato cha kukuwezesha kuendesha maisha yako kwa namna unavyotaka wewe yaende.

Kutokua na fedha ndiyo iwe sababu ya wewe kufanya kazi na kujituma zaidi kuliko kuwachukia wenye fedha na kuisema fedha vibaya.

HAKUNA ubaya wowote kwenye fedha, ni mpaka pale unapokuwa huna fedha na maisha yanakuwa magumu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: