Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kimbia Haraka Sana Ukisikia Neno Hili

Viashiria vya utapeli viko vingi, na watu wengi wanatapeliwa sana.

Utajisikiaje kama leo ukijua kiashiria kimoja cha utapeli?

Ukisikia neno HAKUNA KUFANYA KAZI, kimbia haraka sana maana hapo kuna dalili za kupigwa.

Ukisikia mtu anakuambia kwamba fursa fulani unapata mafanikio bila ya wewe kufanya kazi kabisa, mwambie asante sana kisha ondoka haraka sana na ikiwezekana kimbia kabisa.

Ni utapeli kwamba, mafanikio yatakuwa makubwa bila ya wewe kusumbuka na chochote kile. Usikubali kutapeliwa fedha zako.

Kila kitu kinahitaji kazi, biashara inahitaji kazi, mahusiano yanahitaji kazi, uongozi unahitaji kazi, malezi yanahitaji kazi. Yaani kifupi ni kwamba, kila eneo la maisha yako, linahitaji kazi hivyo usije ukadanganyika kwamba kuna kitu utakipata bila kuweka kazi.

Rafiki wa kweli ni kazi, endelea kufanya kazi na achana na utapeli wa watu wanaokuambia hakuna kufanya kazi na unapata mafanikio.

Wekeza nguvu, muda na fedha zako kwenye uwekezaji wa maana, uwekezaji ambao utakuletea faida na achana na mambo ambayo hayana uhalisia.

Njia ya kufanikiwa ni kufanya kazi, jitahidi sana na wewe kufanya kazi kwa bidii na utayafikia mafanikio makubwa unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; mafanikio makubwa yanahitaji kazi. Na kadiri unavyotaka kufanikiwa zaidi ndivyo na wewe unatakiwa kuongeza juhudi zaidi.

Kitu cha ziada, kutaka mafanikio makubwa bila ya kufanya kazi ni dalili za uvivu na uzembe. Usikubali kuwa mvivu wala mzembe, ni aibu sana fanya kazi ili upate matokeo unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: