Nitakutafuta nikiwa tayari, ni jibu ambalo watu wengi wanaouza wanakutana nalo sana kwa wateja.
Hakuna kazi ngumu kama ya mauzo kwa sababu mauzo ni kitendo cha mteja kujitenganisha na fedha zake. Hivyo inahitaji kazi kumshawishi mteja mpaka atoe fedha yake kwa amani bila kinyongo.
Fedha ni rasilimali yenye uhaba kwa kila mmoja wetu.
Na kutoa hela kuna uma kweli. Wateja wengi wakiwa hawako tayari kununua kitu watakuambia nikiwa tayari nitakutafuta. Kwa kuwa na wewe hujui, utamwambia sawa.
Kama muuzaji hutakiwi kukubaliana na kile ambacho mteja anakuambia nikiwa tayari nitakutafuta, unapaswa umkamate hapo hapo.
Muulize kabisa, unafikiri lini utakua tayari? Hapo utawakamata wengi, kwa sababu wengi hawana hata majibu sahihi bali wanajibu hivyo kwa sababu huenda wana wasiwasi na huduma unayotoa wanakuwa hawana uhakika pengine kama hela yao watakayotoa watapa kweli kile wanachotaka.
Kwenye kazi ya mauzo, kwa sababu sisi sote ni wauzaji, na kila siku unatoka nyumbani kwenda kuuza kitu fulani ili upate fedha. Haijalishi umejiajiri au umeajiriwa kila mtu kuna kitu anauza kwani hakuna maisha kama huna unachouza.
Unapaswa kujifunza mbinu za mauzo kwa sababu maisha ni mauzo na kila siku upo sokoni kuuza kadiri ya kile unachofanya.
Waondolee wateja wasiwasi waliokuwa nao juu ya biashara yako, wateja wanachotaka ni uhakika na uaminifu tu.
Wateja wakishajisikia amani kwako, wanakuwa huru kutoa fedha zao.
Kazi yako kubwa kwenye kile unachofanya ni kujali maslahi ya wateja wako na angalia wana wasiwasi gani juu ya huduma yako na kisha waondoe wasiwasi na wape uhakika.
Wateja wanataka uhakika na uaminifu juu ya kile unachouza, je, kitakwenda kumsaidia kweli? Je, fedha zake zitakuwa salama?
Hatua ya kuchukua leo;
Unapokutana na mapingamizi kama hayo kwa mteja, unapomuuzia mteja kitu na anakuambia nikiwa tayari nitakutafuta, mkamate muulize lini utakuwa tayari?
Muulize tena, unafikiri nini kinakuzuia usiwe tayari sasa? Wakati mwingine wateja wanakuwa hawana hata sababu za msingi hivyo ukiwauliza swali hilo watajiona hawana sababu ya msingi hivyo watashawishika kukubaliana na wewe juu ya kile unachouza.
Rafiki yangu, maisha ni mauzo, kila siku unapaswa kujifunza namna ya kuwa muuzaji bora, cheza na hisia za watu na siyo fikra, watu wanafanya maamuzi kwa hisia hivyo wewe angalia hisia zao ziko wapi ndiyo utaweza kushinda, ukisema uende kinyume na saikolojia ya mteja nakuhakikishia utashindwa kuuza.
Watu wengi wana vitu vizuri sana, lakini kwanini hawauzi? Kwa sababu hawana masoko, hawajui namna ya kumshawishi mteja kununua. Kuna mambo mengi sana kwenye eneo la masoko na mauzo, kila wiki nitakuwa nakupa somo la masoko na mauzo ili uwe bora kujenga ushawishi na kukubaliana na watu kwenye kile unachofanya.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog