Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jifunze Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Hakuna kitu ambacho binadamu wanapenda kwenye maisha yako kama kuthaminiwa. Hali ya mtu kuonekana ni wa muhimu au wa thamani inawafanya watu wajisikie vizuri sana.

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hakuna kiumbe ambaye hapendi kusifiwa, kila mtu anapofanya kitu kizuri, anakuwa anahitaji kupongezwa au kusifiwa.

Wakati mwingine watu wanavunjika moyo hata wa kufanya kazi kwa sababu tu sehemu anayofanyia kazi hawathamini mchango wake.

Habari njema ni kwamba, kitu muhimu cha kujifunza kwenye maisha yako ni kutambua thamani au mchango wa mtu juu ya kitu fulani.

Unatakiwa kuthamini mchango wa mtu yeyote aliyekusaidia au anayeendelea kukusaidia. Usichukulie poa kwa jambo lolote lile.

Kama umeajiri jifunze kuthamimi au kutambua mchango wa wafanyakazi wako. Waoneshe ni jinsi gani walivyo muhimu kwenye safari ya mafanikio yako.

Wakati mwingine tunafikiri watu wanapata hamasa ya kazi kwa njia ya kupewa fedha tu, tena hamasa inayofanya kazi ni ile ambayo mtu anakuwa anathaminiwa na mchango wake unatambulika katika eneo analofanyia kazi.

Hatua ya kuchukua leo;
Jifunze kutambua au kuthamimi michango ya wengine kwenye maisha yako.

Kama kuna mtu ambaye amekusaidia kuwa hivyo ulivyo leo, mwambie ukweli usimfiche, naye atajisikia vizuri sana na ataendelea na moyo wa kusaidia.

Kitu cha muhimu cha kuondoka nacho hapa ni kwamba jifunze kutambua thamani au mchango wa mtu juu ya kitu fulani. Kila mtu ana ubaya na uzuri wake, lakini wewe angalia mazuri ya mtu kwako na achana na ubaya wake.

Kuwa mtu wa kupongeza pale mtu anapofanya vizuri, unapokuwa unapongeza unakuwa unajisikia vizuri hata wewe mwenyewe na utaongeza nguvu ya ushawishi na kukubaliana nao.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: