Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ingekuwa Wewe Ungefanya Nini?

Kiasili sisi binadamu ni wavivu, ni viumbe ambavyo tunapenda kusukumwa kufanya vitu.

Ni watu wachache sana ambao wana nidhamu binafsi ambao wanaweza kupanga kitu na kufanyia kazi.

Kupanga ni rahisi sana ndiyo maana kila mtu anapanga lakini kufanya imekuwa ni kipengele kingine.

Tunao watu wa mfano ambao wanafanya makubwa sasa unapaswa kuwatumia kama watu wako wa mfano, kwa mfano, kama una ndoto ndogo unapaswa kujiuliza maswali, mbona Elon Musk ana ndoto kubwa ya kutaka watu wakaishi sayari ya maazi?

Kama wewe ni mzembe au mvivu unapaswa kujiuliza mbona Bilionea Elon Musk anafanya kazi sana licha ya kuwa ni Bilionea? Tayari yeye ni mtu tajiri lakini ndiyo anafanya kazi muda mrefu kuliko masikini lakini masikini akishapata hela ya kula haendi tena kufanya kazi kwa sababu hela anayo.

Tunao uwezo mkubwa wa kwenda mbali zaidi ya hapa tulipo sasa ni wewe tu rafiki yangu kujisukuma zaidi.

Dunia haiwezi kukupa kitu chochote kile kama wewe siyo king’ang’anizi. Ukiambiwa hapana moja kwako ona kama vile umeambiwa ndiyo.

Sukuma, sukuma, sukuma mpaka upate unachotaka kwenye maisha yako. Usikubali kuishia njiani, Kama kuna watu wameweza wewe ni nani usiweze?

Hatua ya kuchukua leo; kwenye kila eneo la maisha yako jisukume kwenda juu zaidi, usiridhike kupata matokeo unayopata sasa, kila maarifa unayopata yafanyie kazi.

Kila kitu kinafanya kazi kama ukikifanyia kazi ni mpaka wewe ufanye.
Kazi yako wewe ni kufanya yaani kupanda mbegu, kuwa kama mkulima, unapanda, unasubiri ulichopanda kiote, kisha unapalilia na mwisho unavuna, usiwe na wasiwasi pale ambapo umepanda na huoni mavuno, kuwa na subira kama mkulima maana watu wengi siku hizi wanataka Mafanikio ya haraka na yaani wanataka wakipewa mbinu ifanye kazi hapo hapo na isipofanya wanaacha.

Hebu jifikirie tokea mwaka huu uanze umetulia kwenye kitu gani? Usipande leo kesho unaenda kufukua na kuangalia kama mbegu imeota. Panda kisha achia asili imalizie mchakato wake wewe fanya mchakato wako tu na usiingilie mambo ya asili.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: