Kifupi tu rafiki yangu, maisha ni maumivu, , kwa namna yoyote ile huwezi kukwepa maumivu kwenye hii dunia.
Watu wengi wanapenda kupata vitu bila maumivu, mtu anataka maisha yake yabadilike bila kuweka kazi au juhudi yoyote ile.
Wengi wanajiambia kabisa hawezi kujitesa, na ukishindwa kujitesa kwa sababu ya kupata kitu kizuri utakuja kupata maumivu ya majuto.
Kipi bora, upate maumivu ya nidhamu kwa kujikatalia kitu fulani ili ufanikiwe au usiwe na nidhamu binafsi ujiachie halafu uje upate majuto baadaye?
Watu wengi wanakuwa wanafanya vitu na wanataka kuishia njiani kwa sababu mbali.
Lakini leo ninayo habari njema kwako rafiki yangu, ukiwa unafanya kitu na unataka kuacha kwa sababu mbalimbali basi acha kwa umemaliza kazi na siyo kwa sababu umechoka.
Kila siku kwenye maisha yako, usiache kwa sababu umechoka, acha kwa sababu umemaliza.
Je, unataka kuacha? Unataka kuacha kwa sababu gani? Kama ni kuchoka hiyo siyo sababu acha kwa sababu umemaliza.
Hatua ya kuchukua leo; usiache kwa sababu umechoka, acha kwa sababu umemaliza.
Siri kubwa ya kufanikiwa kwenye maisha, ni kuacha kitu pale ambapo umemaliza na siyo kuchoka. Jisukume kumaliza kazi na siyo kuacha kwa sababu umechoka siyo sababu yenye mashiko.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog