Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sifa Inayolipa Sana Duniani

Mwandishi mmoja wa kitabu cha How I Raised Myself From Failures to Success in Selling alikuwa ni mchezaji wa kikapu, alikuwa anachezea timu moja huko Marekani.

Siku moja kocha wake wa timu ya kikapu akamwita, akamwambia tumeamua kukufukuza katika timu yetu ya kikapu.

Frank akauliza, ni kwa sababu gani mmeamua kunifukuza kazi? Kocha wake akamjibu kwa sababu wewe ni mvivu. Unacheza uwanjani kama vile ni mtu ambaye ni veterani, yaani kama vile umestaafu kucheza kikapu. Unacheza bila hata kujisukuma, hujitumi, huna shauku KUBWA ndani yako.

Frank alikuwa hana njia nyingine ya kumwingizia kipato zaidi ya ile, akamuuliza kocha wake, nini anatakiwa kufanya?

Kocha wake akamwambia popote utakapoenda basi hakikisha unacheza kwa shauku.

Hali ya shauku kama ilivyo kwa lugha ya kiingereza ni enthusiasm yaani God within, shauku ni hali ya kuwa na uungu ndani yako.

Frank alipopata timu mpya, alienda kule na kucheza kwa shauku kubwa, shauku yake ilileta mabadiliko makubwa sana katika timu nzima. Alikuwa mchezaji bora na kuwaambukiza shauku timu nzima na kuleta mafanikio makubwa.

Shauku yake katika timu mpya ilimsaidia kipato chake kukua mara mbili ukilinganisha na mwanzo.

Hapa nataka uondoke na kitu, hakuna sifa inayolipa sana duniani kama shauku.

Kwa chochote unachofanya fanya kwa shauku.

Unapoongea na mtu ongea kwa shauku KUBWA.

Unapoongea na mke, mume, rafiki, watoto, wateja nk tafadhali igiza shauku. Ongea kama mtu ana uungu ndani yako tayari.

Mtu ambaye anafanya kitu bila shauku anakuwa hafanikiwi. Binadamu wanahamasika na mtu ambaye ana shauku KUBWA ndani yake.

Angalia hata katika timu zetu za michezo kuna wachezaji hawana hata shauku, yaani wanacheza kama vile watu waliostaafu, lakini wachezaji wa timu za ulaya wanacheza kwa shauku, wanajua nini wanataka wanajituma.

Tafsiri ya mtu ambaye hana shauku kwangu namuona kama ni mvivu na mzembe. Na hakuna tabia ninayoichukia kwenye maisha yangu kama mtu kuwa mvivu na mzembe.

Jitahidi sana kufanya kazi, acha uvivu na uzembe. Dunia inajengwa na watu ambao wanapenda kufanya kazi kwa shauku.

Kama wewe unafanya biashara na unahudumia wateja kinyonge, jitahidi kuwa na shauku wakati mwingine hauuzi kwa sababu shauku yako ni ndogo sana.

Kila mtu anaweza kuigiza kuwa na shauku na akapata matokeo mazuri, usikubali kuwa mvivu na mzembe halafu maisha yakiendelea kukupiga.

Hatua ya kuchukua leo; Igiza kuwa na shauku mpaka shauku ije yenyewe.
Huhitaji mtaji, bali ni wewe tu kuigiza kama mtu mwenyewe shauku KUBWA.

Jitoe kweli kweli, kuwa na moto wa hamasa ndani yako. Shauku ndiyo inasaidia watu kuweza kukubaliana na wewe kwenye jambo lolote lile.

Siku yako nzima ya leo hakikisha unaigiza kuwa na shauku kubwa halafu jioni kabla hujalala fanya tathmini utaona matokeo mazuri utakayopata.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: