Biashara zote ambazo hazifanyi vizuri tatizo lake moja linakuwa kwenye mauzo. Kama biashara haina mauzo mazuri maana yake haina maisha.
Mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara, yaani pumzi kwenye biashara. Mauzo yanapokuwa vizuri, biashara inakuwa vizuri maana itapata fedha ya kujiendesha.
Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failures to Success in Selling, mwandishi Frank anasema siri muhimu kuliko zote kwenye mauzo ni kujua kitu ambacho mtu mwingine anakitaka sana na kisha kumsaidia kupata kitu hicho.
Katika biashara unayofanya, jiulize ni kitu gani watu wanakitaka sana kisha msaidie kupata kitu hicho.
Watu wana maumivu, sasa kazi yako ni kupiga kwenye maumivu, kazi yako ni kutoa dawa ya maumivu ambayo yanawasumbua watu.
Kama mtu anashinda na wewe ukimsaidia kukipata amekuwa tayari ameshanunua.
Maisha ni mauzo, na kila siku lazima uuze ili maisha yako yaende mbele. Bila mauzo kwenye maisha, maisha hayaendi, kila mtu anategemea kuuza ndiyo aweze kuendesha maisha yake.
Hatua ya kuchukua leo; jua kitu gani ambacho mtu mwingine anakitaka sana kisha msaidie kukipata, kwa kufanya hivyo tayari utakua umemuuzia.
Ukifuata siri hii muhimu, uuzaji utakua rahisi sana kwako. Kazi yako wewe kama muuzaji ni kuwasaidia watu kupata kile wanachotaka na wakishakipata basi watakua tayari kununua.
Kifupi, angalia maumivu ya watu na kisha wape dawa ya maumivu.
Mtu anayeumwa, ukimsaidia dawa ya kuponya ugonjwa wake kwanini akatae kununua? Ukiona mteja hanunui basi unamuuzia kitu ambacho siyo maumivu yake, mtu mwenye maumivu huwa hakatai dawa, jua ugonjwa unaomsumbua mtu na kisha mpe dawa ya kutibu ugonjwa huo.
Kitu kimoja cha mwisho, jua kitu ambacho mtu mwingine anakitaka sana kisha kuwa tayari kumsaidia kupata kitu hicho
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog