Kuna watu aina mbili hapa duniani.
Wapo watu ambao wanayakubali majukumu yao na kuchukua hatua.
Na wapo watu ambao wanayakataa kabisa majukumu yao na kutafuta sababu kwa nini hawawezi kuchukua hatua.
Kifupi rafiki yangu, mafanikio hayajawahi kwenda kwa mtu yeyote ambaye siyo wa kukubali majukumu.
Mafanikio yanawapenda wale wanaokubali majukumu na kuchukua hatua na siyo wale wa kutafuta sababu kila mara.
Kamwe huwezi kukuta mtu aliyefanikiwa akikupa sababu kwa nini hajafanya kitu fulani au kwa nini hajapata kitu fulani, utamkuta tayari anacho. Au anakifanyia kazi.
Hatua ya kuchukua leo;
Maisha ni yako, kubali majukumu yako na kama kuna kitu hukitaki kibadili haraka na chukua hatua zitakazokupeleka kule unakotaka kufika.
Kuwa mtu wa kufanyia kazi kile unachotaka na hiyo ndiyo sifa ya mtu ambaye atafanikiwa. Usiwe mtu wa kutamani bila kufanya, beba maisha yako, yabadilishe vile unavyopenda wewe ili mradi hauvunji sheria za asili na nchi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog