Kwanza unapaswa kujua kwamba watu hawanunui kwa sababu ya bei.
Watu wananunua kwa sababu ya thamani na mapenzi.
Usijidanganye kwamba watu wananunua kwa sababu ya bei kuwa chini.
Kwenye mauzo watu wamekuwa wanajidanganya kwamba sababu za watu kutokununua ni kwa sababu hawana fedha au kitu ni bei ghali.
Hivyo wengi hukimbilia kupunguza bei wakiamini ndiyo watauza zaidi.
Na unakuta hata watu wakipunguza bei bado hawanunui, sababu ni nini? Watu hawanunui kwa sababu ya bei. Bali watu wanaangalia thamani unayowapa na mapenzi yao juu ya kitu hicho.
Wajue wateja wako vizuri kwa sababu kama mtu hela ya kula ni shida unafikiri hata ukimshawishi kununua vitu vya juu ataweza?
Tafuta wateja wenye kuweza kumudu na wauzie thamani na mapenzi ya kile unachouza.
Hatua ya kuchukua leo; mwoneshe mteja thamani anayoipata kwa kununua na angalia mapenzi ya mteja juu ya kile unachomuuzia.
Kwahiyo, watu hawanunui kwa sababu ya bei bali watu wananunua kwa sababu ya thamani na mapenzi yao juu ya kile unachouza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog