Watu ni wazuri sana kwenye sababu.
Waulize watu kwanini hawajafanya au kwanini maisha yao yako hivyo walivyo watakupa sababu.
Ukiwapa watu majukumu fulani usipowapa namba ya kuifikia lazima watakupa sababu.
Na nimekuja kugundua sababu hizi tunazojipa ni sababu za uvivu na uzembe. Yaani sababu ndiyo imekuwa kificho cha watu wengi ambao hawataki kuchukua hatua kwenye maisha yao.
Watu wana sababu nyingi kwenye kufanya vitu vya msingi, lakini vitu ambavyo siyo vya msingi hawana sababu. Watu hawakosi muda wa kula, kupiga mswaki lakini watakuambia hawana muda hata wa kusoma kitabu.
Jitahidi sana kuacha sababu, usiwe mzuri kwenye sababu bali kuwa mzuri kwenye kufanya.
Jali mchakato sahihi na matokeo yatakuja yenyewe.
Kazi yako ni kufanya na siyo kujipa sababu. Sababu hazilipi bili, jitahidi kujituma ili upate matokeo mazuri.
Hatua ya kuchukua leo; nenda kawe mtu wa kuchukua hatua na usiwe mtu wa sababu.
Kumbuka sababu hazikusaidii kulipa bili, usitoroke majukumu yako bali fanya majukumu yako.
Ukipanga kufanya kitu, jitahidi ukifanye kweli na acha kuwa mtu wa sababu.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog