Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako ni kawaida kukutana na makundi ya aina tatu ya watu.
Wapo ambao watakubaliana na wewe.
Wapo ambao watapingana na wewe.
Na wapo ambao hawatajali hata unafanya nini.
Kwenye maisha usifanye kitu kwa kutaka uwafurahishe watu, hiyo ni kazi ngumu ambayo hutakuja kuimaliza kamwe.
Kama kuna chochote unataka kukifanya kwenye maisha yako, basi kifanye kwa sababu kuu mbili.
Moja, kwanza kifanye kwa sababu unataka kukifanya na
Mbili, fanya kwa sababu ni muhimu kwako kufanya na upo tayari kukisimamia maisha yako yote.
Usifanye chochote kwa sababu unataka kuwafurahisha watu au unataka ukubalike na kila mtu.
Hata ukifanya kitu kizuri au kibaya sehemu ya watu hawatakubaliana na wewe. Huwezi kukubaliana na kila mtu hivyo kupigwa ni jambo la kawaida sana.
Hatua ya kuchukua leo; fanya kitu kwa sababu ni muhimu kwako kufanya na ni sahihi kwako kufanya.
Kwahiyo, usiishi maisha yako kwa kutaka kumfurahisha kila mtu au kupendwa na kila mtu, fanya kilicho sahihi, fanya unachotaka kufanya.
Na jiandae kusimama mwenyewe pale mambo yatakapokuwa magumu lakini yakiwa mazuri utakua na ndugu na marafiki wa kila aina.
Endelea kupambana na kusimamia ndoto yako bila kuangushwa na mtu. Kuwa mtu imara ambaye hayumbishwi na dunia kirahisi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog