Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Biashara Inayofanikiwa

Watu wengi wanajua kwamba, biashara inayofanikiwa ni ile ambayo inakuwa bora.

Lakini, biashara inayofanikiwa siyo ile inayokuwa bora,
Bali, ni ile inayokuwa ya kwanza kwenye akili za wateja.

Kazi yako kubwa kwenye biashara yako, ni kuifanya biashara yako ifikiriwe na wateja kwenye akili zao.

Mteja akishaifikiria biashara yako, pale anapokuwa anauhitaji wa kununua kitu, hana sehemu nyingine atakayoenda zaidi ya kuja kwako.

Unapaswa kuifanya biashara yako kuwa ya kwanza, kuwa kitu cha kwanza ambacho wateja wanafikiria wanapotaka huduma au bidhaa unayouza wewe.

Kuna vitu viwili unatakiwa kufanya kwenye biashara yako, moja ni masoko na pili mauzo.

Masoko ni kuifanya biashara yako kujulikana na watu. Kama biashara yako haileti wateja basi jua kuna shida eneo la masoko, kazi yako ni kufanya masoko na kuifanya biashara yako itambulike, biashara yako ikae kwenye akili za watu.

Kama biashara yako haijulikani utapata shida sana kwenye mauzo. Na biashara ikiwa haina mauzo inakuwa na dalili mbaya ya kuweza kufa.

Pambana kuifanya biashara yako ijulikane, hakikisha wale wateja ambao unataka waijue biashara yako wanaijua.

Ukiwa umefanya masoko biashara yako inakuwa ya kwanza kwenye akili za wateja.

Masoko yakifanyika vizuri, basi mauzo yataenda vizuri sana.

Ukishafanya masoko pambana sasa kwenye mauzo maana tayari biashara yako inajulikana kilichobakia ni kuwashawishi wateja kununua.

Hatua ya kuchukua leo; ifanye biashara yako inakuwa ya kwanza kwenye akili za wateja.

Kwahiyo, itangaze biashara yako, biashara ikishajulikana utapata wateja tarajiwa wengi na utawageuza wateja hao tarajiwa kuwa wateja kamili na utawashawishi kununua.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: