Pata picha umewahi kukutana na mambo mabaya na katika maisha yako kiasi kwamba ukifikiria unazidi kuumia zaidi.
Kuna watu walikunyanyasa, kukutesa, kukudhulumu na kukuumiza sana kwenye maisha yako.
Hata ukikumbuka yaliyopita hayataweza kukusaidia kitu, upo hapo ulipo sasa unachagua nini?
Unachagua kuendelea kuzama kwenye yaliyopita au kuangalia wapi unakokwenda?
Shabaha yangu kubwa leo ni kukutaka wewe usizame kwenye yaliyopita kwani yanakufanya usiweke nguvu kwenye mambo yako ya sasa.
Watu wengi wamekuwa wanazama kwenye yaliyopita, kujikumbusha mabaya yote waliyopitia na hilo linawazuia kupiga hatua.
Wengi wanaoangalia nyuma ni wale ambao wameshakata tamaa na maisha yao. Wengine wanatumia matukio ya nyuma kama sababu kwa nini wapo pale walipo sasa au hawawezi kufanya zaidi.
Hatua ya kuchukua leo;
Ili uweze kuwa na maisha yenye furaha, unahitaji kuachana na mambo ya nyuma na kuangalia mbele.
Unapoachana na ya nyuma haimaanishi kwamba unayafuta kabisa, hapana unajifunza kupitia hayo ya nyuma lakini huyatumii kama sababu kwani hupigi hatua.
Elekeza nguvu na muda wako kule unakoenda na siyo kule ulikotoka.
Usikate tamaa na maisha yako, usizame kwenye yaliyopita wala kujisifia kwa yaliyopita kama kujipa faraja, ongea na wakati wa sasa ndiyo una nguvu.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog