Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Kuwa Muuzaji Mzuri, Kuwa Na Tabia Hizi Mbili

Kiasili, kila mtu ni muuzaji.
Kila mtu anauza kila wakati, haijalishi wewe ni nani, kila unapokutana na mtu mwingine, unapoelezea wazo lako, unapotoa maoni yako, unauza kitu muhimu sana, ambacho ni wewe mwenyewe.

Kitendo tu cha kuweza kumshawishi mtu na akubaliana na wewe hapo unakuwa muuzaji. Kwa sababu umeuza mawazo yako kwa wengine.

Kama unatafuta kazi unajiuza wewe ili uajiriwe, na unahitaji kuendelea kujiuza kila siku ili kazi yako iendelee.

Maisha ni mauzo, ili uendelee kuishi unapaswa kuwa na mauzo, kwani hakuna biashara itakayoweza kudumu kama haina mauzo mazuri.

Ili uweze kuwa muuzaji mzuri, unapaswa kuwa na tabia hizi mbili.

Moja, tabia ya kuahirisha mambo. Wauzaji wengi wanakuwa na tabia ya kuahirisha mambo, anapanga anataenda kuuza kitu fulani kwa mteja fulani lakini anaishia njiani.

Ukishakuwa na tabia ya kuahirisha mambo kwenye mauzo haifai. Unahitaji kuwa mtu wa kuchukua kama ulivyopanga na kamwe usiahirishe ulichopanga kufanya.

Mbili, ni hofu. Watu wengi wanashindwa kufanya mauzo kwa sababu ya hofu. Hofu inamzuia mtu kuchukua hatua.

Hofu ambazo mtu anaweza kuwa nazo kama vile hofu ya kukosolewa. Kabla mtu hajaenda kwenye masoko anakuwa tayari ameshajikataa ndani yake.

Watu wanakuwa na hofu nyingi kiasi kwamba wanashindwa kuchukua hatua yoyote kwenye mauzo.

Hatua ya kuchukua leo; ili uweze kuwa muuzaji mzuri unapaswa kujiamini, usihofie chochote hata kama mtu atakataa kununua bidhaa yako hajakukataa na wewe bali ni bidhaa.

Usiahirishe ulichopanga kufanya, kama ni ndiyo au hapana acha uisikie kutoka kwa yule mhusika. Kazi yako ni kuuza na kununua waachie wateja ndiyo wenye maamuzi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: