Wazazi wa siku hizi wanawalea watoto utafikiri wamepata mkataba wa kuishi nao milele.
Wazazi hawataki kuwafundisha watoto kukosa. Mtoto akitaka kile anachotaka anapewa mara moja. Hii inamfanya mtoto kuja kuteseka baadaye anapokuja kuingia kwenye uhalisia wa mambo.
Watoto wanaharibiwa kwa kukosa adhabu kuliko kuharibiwa na adhabu. Kumekuwa na harakati nyingi za kufuta adhabu kwa watoto kuanzia majumbani mpaka mashuleni.
Lakini ukikaa chini na kutafakari vizuri kwa undani unaona jinsi adhabu zinawasaidia watoto kuelewa uhalisia wa dunia.
Kwa sababu bila adhabu, watoto wanakua wakijua kwamba dunia inapaswa kuwasikiliza wao, inapaswa kuwapa kila wanachotaka.
Wanakuwa wakiwa na mtazamo mbovu na wakiwa na mazoea mabaya hivyo vinawafanya washindwe kufanikiwa kwenye maisha yao.
Hatua ya kuchukua leo; usiwanyime watoto adhabu, pale anapokosa mpatie adhabu ili ajifunze uhalisia wa maisha.
Licha ya mapungufu ya adhabu, lakini zinawasaidia watoto, zinawafanya watoto wajenge tabia nzuri na wajiandae kukabiliana na dunia.
Adhabu za dunia ni kali kuliko zile zinazotolewa na wazazi. Dunia inadhibu kwa ukatili kuliko hata wazazi wanavyoadhibu.
Usipomfundisha mtoto wako mapema, dunia itakuja kukusaidia kumwadhibu kwa riba na kwa ukatili sana bila huruma. Kama unampenda mtoto wako, mfundishe uhalisia wa maisha jinsi ulivyo. Haijalishi una kipato kikubwa au kidogo malezi hayaangalii hayo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog
Elimu ni nzuri Sana juu ya makuzi ya Watoto.
LikeLike