Angalia faida.
Kwenye mauzo yoyote yale unayofanya angalia faida.
Faida ndiyo kila kitu kwenye biashara, usifanye biashara kwa hasara kwa sababu hasara haitakusaidia kulipa bili wala kuendesha biashara yako.
Unapofanya mauzo, kitu cha kwanza kufanya ni kuchukua mauzo kutoa gharama za mauzo. Kile kinachobakia sasa ndiyo faida yako halisi.
Na ili upate faida nzuri, hakikisha mauzo yako yanakuwa juu. Ukiona unapata faida kidogo, jipe changamoto ya kuongeza mauzo ili upate faida kubwa.
Hakikisha idadi ya manunuzi anayofanya mteja yanakuwa juu, mshawishi mteja anunue bidhaa zaidi ya moja. Hii itakusaidia kuongeza mauzo yako na kupata faida.
Mteja akinunua mara moja ni hasara. Usikubali mteja anunue mara moja tu kwako, hakikisha anaponunua mara moja arudi tena kununua mara ya pili. Kwa mfano, unauza magari, mteja amekuja kwako kwa ajili ya kununua gari, ukimwambia mteja ukinunua gari kwetu tunakujazia mafuta “full tank” atashawishika kununua na siku nyingine pia atashawishika kurudi tena.
Hatua ya kuchukua leo; Kwenye kila mauzo unayofanya kwenye biashara yako, hakikisha unaangalia faida yako ni shilingi ngapi.
Usifanye mauzo kwa hasara, kwenye kila mauzo hakikisha unapata faida. Faida ndiyo uhai wa biashara yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog