Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Kinachomfanya Mtu Achukue Hatua Haraka

Huwa tunalalamika kwanini watu wengine tukiwaambia wafanye kitu fulani hawachukui hatua.
Siyo tu watu wengine, wakati mwingine hata sisi wenyewe tunakuwa ni wagumu kuchukua hatua.

Unafikiri ni kwanini watu wanakuwa wagumu kuchukua hatua? Kwa sababu hujagusa maslahi yao binafsi.

Kitu kinachomsukuma mtu kuchukua hatua haraka ni maslahi. Mtu anakuwa ana hamasika kuchukua hatua pale anapokuwa anaona kuna maslahi fulani anayapata.

Kwa mfano, tunayo mambo mengi ya kufanya na muda wetu ni mchache lakini yale mambo ambayo yana maslahi kwetu huwa tunayapa kipaumbele na tunasukumwa kuyafanya kwa haraka kwa sababu tunajua kuna maslahi tunapata.

Ukitaka mtu afanye kitu chochote kile kwa haraka hakikisha kuna maslahi fulani anapata. Kama watu hawana wanachopata huwa hawajitumi sana.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka watu wasukumwe kuchukua hatua fulani basi hakikisha kuna maslahi fulani wanayapata.

Maslahi ndiyo kitu kinachomsukuma mtu kuchukua hatua. Binadamu ni watu wa maslahi binafsi, ukitaka kukubaliana nao kwenye maeneo mengi basi hakikisha unagusa maslahi yao binafsi ndiyo utaweza kuwapata kiurahisi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: