Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mchezo Unaongoza Kuchezwa Na Watu Wengi

Ni mchezo wa kulaumu.

Huwa tunashiriki mchezo wa kulaumu, kwa kuangalia mtu wa kumnyooshea kidole ambaye anahusika na kile ambacho kimetokea.

Tatizo lolote lile linapotokea, huwa tunatafuta mtu wa kumlaumu na mara nyingi mtu wa kumlaumu huwa hakosekani kabisa.

Lakini, kwenye kila tunacholaumu, huwa tunajionesha sisi zaidi kuliko hata wale tunaowalaumu..

Tuache kuangalia wengine kama sababu, ili kuthibitisha imani ambazo sisi tunazo juu ya wengine.

Kumbuka kwamba, unapolaumu, jua shida siyo yule unayemlaumu, bali wewe unayelaumu ndiye mwenye shida hasa kama hujaelewa vizuri kile kilichotokea.

Acha kushiriki kwenye mchezo wa kulaumu badala yake, wajibibika kwenye nafasi yako na ile ambayo iko nje ya uwezo wako achana nayo. Kile ambacho unaweza kufanya, kifanye vizuri na kile ambacho huwezi kufanya waachie wengine wanaoweza au wenye mamlaka makubwa kwenye eneo hilo kuliko kushiriki kwenye mchezo wa kulaumu.

Hatua ya kuchukua leo; ili kuondoka na silika ya lawama, usiangalie mtu mmoja au kitu kimoja kilichosababisha, bali angalia mwingiliano wa vitu ambao umesababisha kilichotokea na siyo kulaumu mtu mmoja.

Kwahiyo, iko mifumo ambayo inafanya mambo kutokea na wakati mwingine mambo yanatokea tu hivyo vitu vingi vinatokea kwa sababu kuna mifumo imara au dhaifu na siyo kwa sababu ya maamuzi ya mtu mmoja.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: