Kinachotusumbua kwenye maisha, ni pale tunapojilinganisha na wengine na kuona kwa sababu wengine wana zaidi, basi na sisi tunapaswa kuwa na zaidi.
Tunajikuta tunakazana kupata zaidi, siyo kwa sababu tunahitaji kweli ila ni kwa sababu wengine wana zaidi.

Haya ni mateso ya kujitakia kwenye maisha, ya kutaka kupata vitu ambayo hata siyo muhimu kwako.
Unapaswa kujua vile vitu muhimu vinavyofanya maisha yako kwenda. Kisha usikubali vingine vikusumbue kwa sababu siyo muhimu kwako.
Kila mtu ana vitu ambavyo ni muhimu kabisa kwenye maisha yake, kama vile chakula, malazi, mavazi, afya na elimu ni vitu ambayo ni muhimu kwa kila mtu.
Na kila mtu ana kiasi katika vitu hivyo ambavyo vinafanya maisha yake kwenda vizuri.
Kiasili mahitaji ya msingi ni machache tu, ila anasa ndiyo zinafanya maisha kuwa magumu na kujitesa.
Hatua ya kuchukua leo;
Usijilinganishe na wengine na kubali maisha yako yaende kadiri ya vile muhimu ulivyonavyo vinavyofanya maisha yako yaende na siyo vinginenvyo.
Kwahiyo, usikubali kujitesa na kuishi maisha ya mateso ya kuhangaika sana na vile vitu ambavyo hata siyo muhimu kwako kwa kuhangaika kuwa navyo kwa sababu umemuona fulani anacho na wewe unataka kupata zaidi.
Epuka sana kujilinganisha na wengine kwani kujilinganisha ni mwizi wa furaha yako. Hakuna anayejilinganisha na mwingine halafu akabaki salama.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog