
Mahusiano yetu yanakuwa magumu wakati mwingine kwa sababu kuu moja ambayo ni kukosa mawasiliano.
Kama unavyojua kitu kikiwa kigumu kinatakiwa kilainishwe ili kupatikana kwa ulaini.
Mahusiano yetu yanakuwa magumu endapo yakikosa mawasiliano mazuri. Kitu ambacho kinaweza kulainisha mahusiano yetu ni mawasiliano na wale ambao tunahusiana nao.
Kila unayehusiana naye anahitaji muda wako na usipompatia muda wako unafanya mahusiano kuwa magumu. Jijengee tabia ya kutenga muda hata kwa wiki moja kwa ajili ya mawasiliano na wale watu wako wa karibu.
Mawasiliano yatakusaidia kujua nini kinaendelea kupitia yule unayehusiana naye. Kuna mengi tu ambayo utakua hujui kupitia yule unayehusiana naye lakini ukitenga muda na kumsikiliza utajua yale anayopitia na kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali.
Chochote kile ambacho unakipa muda lazima kitakupa matokeo mazuri na kile ambacho hukipi muda hakitakupa matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.
Mawasiliano yatakusaidia kujenga ushawishi na kuimarisha mahusiano yako na yule unayehusiana naye.
Angalau kila siku jitahidi hata kuwatumia ujumbe watu 5 au kuwapigia wale ambao ni watu wako wa karibu kuwajulia hali. Usisubiri mpaka mtu apate tatizo ndiyo uje uwasiliane naye. Ukiwa unawasiliana na mtu mara kwa mara utajua nini anapitia.
Mahusiano ya watu wengi yanakuwa magumu kwa sababu ya kukosa mafuta ya kuyalainisha na mafuta ya kulainisha mahusiano yako ni mawasiliano.
Fanya kazi lakini usisahau kujenga mahusiano mazuri na wale unaohusiana nao. Unaweza ukawa mtafutaji mzuri lakini kama hata hupati muda wa kukaa na familia yako utajikuta unajitengenezea matatizo mengi.
Kumbuka mahusiano yanahitaji muda na kila mmoja anahitaji kuonekana anaheshimiwa na kuthaminiwa katika mahusiano ambayo upo.
Hatua ya kuchukua leo; lainisha mahusiano yako kwa njia ya mawasiliano. Wasalimie watu unaohusiana nao, wateja unaofanya nao kazi na wale wote ambao wanajihusisha na wewe kupitia kile unachofanya au huduma unayotoa.
Jenga urafiki na watu kwanza ndiyo utaweza kunufaika nao. Kuliko kutaka kitu kwao huku ukiwa huna mahusiano mazuri na wao.
Mahusiano yanajengwa na mawasiliano. Wape muda wale wote ambao unahusiana nao itakusaidia kujenga ushawishi na kuimarisha mahusiano yako na wale wote unajihusisha nayo au kuhusiana nao.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog