Design a site like this with WordPress.com
Get started

Dunia Itafanya Njama Na Wewe

Pale unapojitoa kweli kupata kile unachotaka kwenye maisha yako, dunia inakuwa inafanya njama na wewe kuhakikisha unapata kweli kile unachotaka kwenye maisha yako.

Jitoe sana kwenye kile unachotaka hata kama hujui utapateje lakini wewe amini, nia yako na uthubutu wako utaifanya dunia kufanya njama na wewe upate kile unachotaka.

Amini kweli, kila kitu kinawezekana kama ukijitoa kweli.
Unapoweka malengo ya kitu, na dunia inaona juhudi zako na ung’ang’anizi unaoweka kwa nini sasa isikupe kile unachotaka?

Dunia itatafuta watu wa kufanya nao njama ili uweze kupata kile unachotaka.

Kazana mpaka upate kile unachotaka, safari ya mafanikio siyo rahisi ila ukijitoa dunia itafanya njama na wewe kuhakikisha unapata kile unachotaka.

Kila wakati fikiria kupata kile unachotaka, vuta picha ya kile unachotaka, ona tayari kipo mikononi mwako, andika mara kwa mara au kila siku kile unachotaka utakipata kweli.

Haijalishi unapitia hali gani, wewe ukishakuwa tayari na kujitoa bila kujibakiza dunia itafanya njama na wewe kuhakikisha unapata ushindi wako.

Wakati mwingine tunashindwa kupata ushindi kwenye maisha yetu kwa sababu ya kukosa ung’ang’anizi, wengine wakipata changamoto kidogo tu wanakubali kujipa kibali cha kushindwa na kuishia njiani.

Usikubali kujipa kibali cha kushindwa, jipe kibali cha kushinda.

Wanaopata ushindi ni wale wanaokomaa na safari mpaka mwisho. Usiishie njiani, maliza kile ambacho umekianza ndani yako.

Usiwe kama mkulima kichaa, anayepanda leo na kwenda kufukua kesho kuangalia kama kile alichopanda kimeota.

Wekeza ila kuwa na subira ya kupata ushindi kwenye uwekezaji uliofanya.

Unachotakiwa kufanya ni wewe kuwa katika mchakato sahihi na matokeo yako nje ya uwezo wako.

Hatua ya kuchukua leo; Jitoe kweli kwenye kile unachotaka na dunia itafanya njama na wewe kuhakikisha unapata kweli kile unachotaka.

Kuwa katika mchakato sahihi, dunia itakupa kile unachotaka kwenye maisha yako. Jitoe kweli na dunia itakuwa tayari kufanya kazi na wewe kuhakikisha unapata kweli kile unachotaka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: