Design a site like this with WordPress.com
Get started

“Kwa Mkapa Hatoki Mtu”

Ni kauli ya hamasa ambayo klabu ya Simba nchini Tanzania huwa wanaitumia pale wanapokuwa wanacheza na timu inayotoka nje ya Tanzania.

Pata nakala yako leo kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 5, kupata kitabu chako wasiliana nasi kwa namba 0717101505/0767101504

Imekuwa ni kauli ambayo huwa inawapa hamasa na hatimaye wanaitumia vizuri sana kuhakikisha hakuna timu inayowafunga nyumbani kwao.

Kitu kikubwa ambacho nimejifunza kwenye maisha ni kwamba watu wanahitaji hamasa sana ili kuchukua hatua. Ili watu waoneshe uwezo mkubwa uliopo ndani mwao wape hamasa na utaona makubwa wanayokufanyia.

Hakuna mtu ambaye hawezi kufanya ila watu wamekosa hamasa ya kufanya. Ukipata mtu ambaye atakutia hamasa utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Hata wewe unaweza kuwa na kauli mbiu inayokuhamasisha kupata kile unachotaka kwenye maisha yako, kwa mfano, Simba wanapocheza na timu nje kwenye uwanja wao wa nyumbani wanatumia kauli hii “kwa Mkapa Hatoki Mtu” hii inamaanisha kuwa watapambana kuhakikisha wanapata ushindi au wafe wakiwa wanapambania ushindi.

Klabu za mpira wa miguu nyingi huwa zina kauli mbiu zao, mfano, Klabu ya Yanga wanayo inayosema “Yanga mbele daima, kurudi nyuma mwiko”

Kila kitu kinawezekana. Jipe changamoto za kufikia mafanikio fulani unayotaka kisha tafuta kauli mbiu ambayo itakusukuma kufikia mafanikio hayo. Kwa mfano, kwenye eneo la fedha unaweza ukajiwekea malengo labda mwezi fulani lazima niingize kiasi fulani cha fedha, baada ya kuwa na hiko kiwango utapata hamasa ya kukusukuma, kuweka juhudi hatimaye kufikia lengo lako.

Usichukulie poa kuhusu hamasa kwa sababu binadamu ni viumbe vya hisia hivyo wanahitaji hamasa sana ili kuweza kuonesha uwezo wao, amsha uwezo ulio lala ndani yako kwa kujipa kauli za hamasa.

Kwenye klabu ya Mimi Ni Mshindi Nimezaliwa Kushinda, tuna kauli za hamasa ambazo tunazitumia kujihamasisha. Zipo kauli nyingi ambazo kila mmoja wetu amechagua ya kwake kwenye semina ambayo atatembea nayo pale anapojihisi amekosa hamasa basi anajibusti kidogo.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa na kauli mbiu inayokuhamasisha kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.

Jifunze hata katika kampuni kubwa duniani zina kauli mbiu, kwa mfano Nike wanayo kauli yao inayosema just do it. Mtu yeyote anayefanya kazi kwenye kampuni hiyo pale anapokuwa anataka kuahirisha jambo anakumbuka kauli ya just do it, ni kauli mbiu ambayo haina sababu bali inataka matokeo tu.
Hata mimi napotaka kuandika, huwa sina sababu bali nakaa chini naandika.

Kwenye maisha kama utaleta sababu, huna hamasa, huna kauli mbiu inayokuchochea kuchukua hatua kwenye jambo lolote lile unalofanya utajikuta hutokei kwenye kitu chochote kile.

Jipe hamasa, tengeneza kauli mbiu ambayo itakusukuma kuchukua hatua na hatimaye kufikia mafanikio uliyojiwekea kupata.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: