Njia bora kabisa ya kuwapenda watu ni kuwakubali kama walivyo.
Kila mtu ana tabia zake, kila mtu ana upekee wake, uimara na udhaifu wake.

Tunaweza kunufaika na wale watu wetu wa karibu kwa kuwapenda kama walivyo.
Aliyekuwa raisi wa Marekani Abraham Lincoln aliwahi kunukuliwa akisema, ukitafuta ubaya kwa mtu tegemea kuupata. Kazi yetu siyo kutafuta ubaya, bali ni kuwapenda jinsi walivyo. Ni nani ambaye hana udhaifu? Nani akitafutwa kadiri ya udhaifu wake atabaki salama? Hakuna.
Ukishaanza kusema unawapenda watu kwa sababu wako kwa aina fulani, na ukishaanza kutaka watu wabadilike na kuwa kama unavyotaka wewe ndiyo uwapende, jua hapo hujawapenda watu.
Haitatokea kila mtu kwenye maisha yako kuwa kama unavyotaka wewe.
Na kiasili, watu hawatabadilika kwa namna unayotaka wewe.
Hapo utakua unatafuta cheo cha kuwa kiranja wa dunia cha kutaka watu waende kama unavyotaka wewe.
Unapaswa kujua;
Kila mtu ana utofauti wake,
Ana changamoto zake,
Na pia,
Ana mchango fulani katika maisha yako.
Hakuna mtu ambaye hana msaada hapa duniani, kila mtu ni zawadi, jifunze namna ya kutumia kila zawadi ambayo Mungu anakukutanisha nayo.
Hatua ya kuchukua leo; ondoka na sentensi hii moja kwamba, njia bora ya kuwapenda watu na kujenga maji bora ni kuwakubali kama walivyo, bila kutaka wabadilike au wawe kama unavyotaka wewe.
Kwahiyo, hata Mt. Agustino wa Hippo enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema, kipimo cha upendo, ni kupenda bila kipimo.
Hivyo wapende watu kama walivyo, nufaika na uimara walionao na udhaifu achana nao maana hautakusaidia zaidi ya kukuumiza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog