Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ili Uweze Kufanikiwa Kwenye Safari Ya Mafanikio Makubwa Lazima Mwenza Wako Akupe Kitu Hiki

Watu ambao wako kwenye ndoa huwa wanakutana na upinzani mkubwa hususani pale mmoja wa ndoa anatapotaka kuthubutu kitu au anapokuwa na ndoto kubwa.

Kikawaida jamii zetu hawapendi kuona mtu akiteseka kwa mfano, ukimwambia mtu kwamba unataka kwenda kufungua biashara na yeye hafanyi biashara atakuambia biashara ni hatari, usijitese. Na watakuambia hivyo ili mradi tu wasikuone unapata tabu.

Kadiri ya uzoefu wangu wa huduma ya ushauri na maarifa ya ndoa ninaotoa nimekutana na mengi na leo ninaona bora nikushirikishe.

Ni wanandoa wachache sana katika zama hizi ambao wanashirikiana pamoja katika malengo makubwa ya pamoja. Mke na mume ambao wamekuwa kitu kimoja lakini cha ajabu hawana hata umoja zaidi ya ubinafsi. Kila mmoja anajua mambo yake na ikitokea mmoja ana ndoto kubwa ndiyo shida huwa inaanzia hapo.

Safari ya mafanikio makubwa ni ngumu, kuna changamoto za kila aina hivyo basi ili uweze kufanikiwa kwenye safari ya mafanikio mwenza wako anapaswa akupe ushirikiano wa kutosha.

Lakini pia akuelewe na kukutia moyo pale unapopitia magumu. Kama mwenza wako hayuko upande wako safari ya mafanikio kwako itakua ni ngumu. Kusaka mafanikio ni vita, na unapokuwa vitani yeyote ambaye hayuko upande wako huyo ni adui wako. Sasa kama mwenza wako hayuko upande wako anakuwa adui yako.

Kiasili sisi binadamu huwa tunakuwa tunaelewana sana na yule mtu ambaye anakuwa upande wetu. Mtu ambaye anakuwa hayupo upande wetu anakuwa ni kama vile adui yako.

Kwenye safari hii ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa, mwenza wako anapaswa kuwa upande wako asilimia 💯 la sivyo kuna kimoja kitashindikana.

Kwa mfano, kama kimoja kitashindikana huenda ikawa hivi, labda hutafanikiwa kabisa au mahusiano hayatawezekana.

Kila mmoja wetu anapaswa kulijua hili kwa uwazi kabisa na kuhakikisha mwenza wake pia analijua kwa uwazi kabisa maana bila hivyo mtaishia kusumbuana tu.

Ni wenza wa chache sana ambao wanawavumilia wenza wao na wale ambao hawana subira mara nyingi maisha yanawashinda wanatafuta sehemu nyingine ambayo watapata mafanikio ya haraka.

Hatua ya kuchukua leo; kaa chini na mwenza wako mueleze ndoto ulizokuwa nazo na faida kubwa utakazopata pale utakapofanikiwa kukamilisha ndoto hizo.

Muelewe mwenza wako pale anapokushirikisha ndoto kubwa alizonazo na mshike mkono.
Kuwa upande wa mwenza wako kuhakikisha kila alichoamua kuthubutu unakuwa upande wake.

Acha wivu wa kimapenzi kwa kuhofia mwenzako wako atabadilika, kumbuka mahusiano hayaendi bila fedha na wivu haulipi bili hata uwe na wivu kiasi gani hautakusaidia kufanikiwa kwenye ndoto kubwa. Hivyo, kila mmoja aingie uwanjani kupambana na kucheza namba yake vizuri.

Wanandoa wanaoishi umoja hakika asili huwa inawabariki. Asili ya ndoa ni umoja sasa watu wengi wanaenda kinyume ndiyo maana mapigo hayaishi kwenye ndoa nyingi.

Kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mwenza wako maana mafanikio yako, mafanikio yake, na aibu yako aibu kwake. Kwa mfano, wanawake ambao wako kwenye ndoa na wana ndoto kubwa waume zao ndiyo wanakuwa watu wa kwanza kuwapinga, wanapitia changamoto nyingi, wanafikiria kama mwanamke akifanikiwa huenda akapoteza umiliki wake. Usiwe na hofu, kila mmoja ampe mwenza wake nafasi ya kujaribu na mtiane moyo kwani umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: