Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Kinachokupelekea Kuwa Na Laana

Kinachokupelekea wewe kupata laana ni tabia zako.

Unapata laana kwa ajili ya tabia zako mwenyewe. Kwa sababu unatengeneza tabia kisha na tabia zinakutengeneza.

Kwa mfano, unatengeneza tabia za uvivu kwenye maisha yako, hujitumi halafu baadaye hufanikiwi unasema unalaana, huna bahati kumbe chanzo kikuu ni tabia ulizojijengea.

Kwa mfano, wazazi wengi huwa wanaangalia tabia za watoto jinsi walivyo, na baada ya hapo huwa wanasema kabisa, kwa mwenendo huu, sidhani kama utafanikiwa kwenye maisha yako, na kweli mtoto anakuja kutokufanikiwa baadaye, unaweza kuona mzazi ametoa laana kumbe, mzazi ameshaona mwenendo wa tabia za yule mtoto.

Kumbe basi, tabia ndiyo zinapelekea wewe kupata laana fulani kwenye maisha. Kwa mfano, ukiangalia mwenendo wa mtu anavyofanya kazi unajua kabisa huyu lazima atapandishwa cheo au kushushwa cheo.

Huwa tunatabiri vitu vingi kwa wenzetu kupitia tabia walizonazo. Kwa mfano, mtoto akiwa na mwenendo mbaya labda amekuwa ni mwizi wa vitu vidogo vidogo, mzazi anaweza kusema kwa tabia yako hiyo ya udokozi utaishia jela tu. Hapo unaweza kuona kama mzazi ametoa laana ila ametoa maoni hayo kutokana na tabia alizonazo huyo mtoto, kwa kuona mwenendo wa maisha yake anajua wazi kule atakapoishia.

Kwa mfano, mwalimu anajua kabisa kwa tabia za mwanafunzi fulani zilivyokuwa nzuri, zitamsaidia kufika mbali kwenye masomo yake ya juu. Na mwanafunzi akiwa na tabia ambazo siyo nzuri mwalimu anasema kabisa kwa tabia za mwanafunzi fulani haziwezi kumfikisha mbali. Hapo mwalimu hajatoa laana bali tabia za mwanafunzi ndiyo zimepelekea mwalimu aseme kile alichokisema.

Kwa mfano, kwenye michezo, mchezaji anapofanya vizuri watu wanamtabiria mema, kwa tabia yake na jinsi anavyocheza lazima atafika mbali.

Kumbe basi, tabia zako ndiyo zinapelekea watu kukusemea vitu vya laana au baraka. Kwa chochote unachofanya watu watakuhukumu kutokana na tabia yako.

Hatua ya kuchukua leo; vunja tabia zote mbaya zinazoweza kukupeleka kwenye laana na Jenga tabia bora kabisa zinazoweza kukupeleka kwenye bahati, mafanikio makubwa na hata matashi mema kutoka kwa watu.

Kwahiyo, tabia ndiyo inakupelekea kuwa na laana au bahati. Jenga tabia bora ili tabia bora zikutengeneze na kuwa bora.
Kumbuka kuwa, tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga, je, unajengeka tabia gani?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: