Design a site like this with WordPress.com
Get started

Unaamini Kama Ninavyoamini Mimi?

Ukitaka kujua watu hawana imani na kile wanachotaka kwenye maisha yao angalia imani yao kwenye utendaji na uzungumzaji.

Kifupi watu wameyafunga maisha yao kwenye gereza la imani.

Watu hawana imani thabiti, wanaamini midomoni ila hawaamini kwenye vitendo.

Unakuta mtu ana ndoto kubwa lakini hana imani kama inawezekana.

Asikuambie mtu ukiwa na imani huwezi kushindwa kitu chochote kwenye hii dunia. Kama unaishi ulimwengu wa imani basi utakua unaishi kwenye dunia salama.

Wote tupo duniani lakini kila mmoja wetu anaiona dunia kwa utofauti wake. Ukivaa miwani nyeusi utaiona dunia ni nyeusi hivyo basi, kwenye maisha ni vile unavyoamini wewe je unaamini kweli utafanikiwa kupata kile unachotaka kwenye maisha yako? Au umeweka malengo lakini imani yako ni ndogo?

Wote tunalijua gari, na gari huwa haliwezi kwenda lenyewe bila nishati ya mafuta, ila ukiweka nishati na kuliendesha litaenda. Ninashangaa watu wanataka kuendesha magari huku wakiwa hawana hata mafuta.
Hapa ninamaanisha kuwa wengi wana ndoto lakini hawana imani kama inawezekana katika hali ya kawaida.

Falsafa mpya ambayo ninakusihi uwe nayo kwenye maisha yako ni kwamba, kila kitu kinawezekana, haijalishi una kitu fulani au huna ukiamua kila kitu kinawezekana.

Ukitaka kupunguza matatizo kwenye maisha yako, kuwa na imani. Kwanini uwe na imani?
Kwa sababu imani inaondoa mipaka yote.

Maisha yako yanashindwa kufunguka kwa sababu ya imani uliyokuwa nayo. Unajifunga kiroho, kiakili na kimwili. Kila kitu unaona hakiendi ni kwa sababu ya imani uliyokuwa nayo.

Imani inafungua njia za milango ya baraka. Ukiamini na kujinenea mambo mazuri na kuwa chanya muda wote utaona ukuu wa Mungu ndani yako.

Kama huna imani huwezi kupokea chochote kile, akili yako ikiamini kitu na kukipokea, lazima itafanikiwa kukipata. Sikufichi amini hilo. Kwa sababu mchezo mzima wa mafanikio uko kwenye akili yako.

Ukiamini leo utapata matokeo mazuri kwenye kazi, biashara au kile unachofanya utapata kweli lakini ukiamini tofauti huwezi kupata kile unachotaka.

Hatua ya kuchukua leo; lazima imani yako iendane na matendo yako.

Kuwa na imani kwamba kila kitu kinawezekana, amini kwamba chochote kile ambacho akili yako itakiamini na kukipokea itafanikiwa kukipata.
Hata kama umesahau yote ondoka na sentensi hiyo moja tu hapo juu.

Nenda kaondoea vizuizi vyote ulivyojiwekea kwenye maisha yako kwa njia ya imani. Ukiamini huwezi utapata matokeo ya kushindwa na ukiamini unaweza utapata matokeo mazuri ya kuweza.
Imani inakupa kile unachokiamini je, unaamini kama ninavyoamini mimi? Kwamba kila kitu kinawezekana kama akili yako ikiamini na kukipokea kitu lazima utafanikiwa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: