Urafiki ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu. Na zana ya kujenga na kuimarisha mahusiano ni mawasiliano.
Mwanafalsafa Aristotle enzi za uhai wake alisisitiza sana umuhimu wa urafiki kupitia maandiko ya kifalsafa.
Na alifanikiwa kugawa urafiki kwenye ngazi tatu.
Ngazi ya kwanza ni urafiki wa faida au urafiki wa nipe nikupe.
Huu ni urafiki ambao unajengeka pale watu wanapokuwa na manufaa wanayoweza kuyapata kwa wengine.
Huu ni ule urafiki wa juu juu, mtu anauanzisha ili apate kitu fulani kutoka kwako. Ni urafiki ambao kila mtu anakuwa ana maslahi yake binafsi.
Na aina hii ya urafiki huwa haudumu kwa muda mrefu maslahi yakishaifa na mtu akishapata kile anachotaka urafiki unakua unakufa.
Urafiki wa raha (bata). Aina hii ya urafiki unajengeka kwa watu ambao wanapata raha na starehe kwa pamoja.
Urafiki huu unakuwa wa kukutana kwenye bata tu, watu wanakutana kwa ajili ya kula maisha wakati wa mapumziko au starehe kwa mfano, kuangalia michezo au sinema pamoja, kunywa pamoja nk.
Aina hii ya urafiki hauna nguvu kubwa kwa sababu starehe zinapokosekana na urafiki unavunjika. Urafiki huu unakuwa hauna hata msaada kwani mtu anapokuwa anapitia magumu urafiki wa aina hii unakuwa hauna msaada kwake.
Huu ni urafiki wa raha tu na watu hawataki kusikia shida zako. Ni urafiki ambao wala hauhusiki na shida zako, kiufupi ni urafiki wa raha tu.
Ngazi ya tatu ya urafiki ni urafiki wa tabia. Huu ni urafiki wa kukubaliana na kuaminiana.
Ni urafiki ambao watu wanakuwa wameelewana, kukubaliana na kuaminiana kulingana na tabia ambazo mtu anazo.
Watu wanakuwa tayari kushirikiana wakiwa na tabia zinazoendana karibu kwenye mambo mbalimbali ya kimaisha.
Kinachowaleta watu karibu ni tabia zao na zinakuwa na nguvu na siyo madhaifu yao.
Hatua ya kuchukua leo; Kuwa na urafiki wa tabia na achana na aina nyingine za urafiki ambao ni bata na nipe nikupe.
Kwa nini nakushauri ushauri wa tabia? Kwa sababu ni urafiki unaoweza kudumu kwa muda mrefu kwani watu wanakuwa wanasukumana kupeana ushauri, hamasa na hatimaye mtu kuwa bora.
Na ni aina ya urafiki ambao kila mmoja anakuwa anajali maslahi ya mwenzake, na siyo kuangalia yeye anapata nini, huu ni urafiki ambao kila mtu ana shinda. Kila mtu anataka mwenzake atoke na awe bora. Ni urafiki mzuri wa kusaidiana na ni urafiki wa faida kwani kila mmoja ananufaika na kuwa bora.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog