Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kuwa Mtu Wa Namna Hii Kama Unataka Kupiga Hatua Kubwa

Iko kauli moja ambayo nimejifunza hivi karibuni inayosema, ni rahisi kuyavumilia maisha magumu kuliko kupambana kupata maisha bora.

Unapata nini kwenye kauli hiyo? Hapo anamaanisha kwamba, ni kazi zaidi kupambana kupata maisha bora kuliko kuvumilia maisha magumu.

Hii iko wazi kabisa kwenye maisha, angalia watu wengi wana maisha magumu na hakuna hatua za tofauti wanazochukua unafikiri ni kwa nini? Kwa sababu hawataki kujitesa zaidi, wanapenda kuwa na maisha mazuri lakini hawachukui hatua wanaendelea kuvumilia maisha magumu.

Usivumilie maisha magumu, pambana uvuke ugumu huo na wala usilalamike, kama iko ndani ya uwezo wako fanya maamuzi sahihi na utaweza kupiga hatua zaidi.

Kama unataka kufanikiwa au kupiga hatua kwenye maisha yako, kitu cha kwanza unachopaswa kufanya ni kuwa mkweli kwako mwenyewe.

Watu wengi wanaigiza maisha, siyo wa kweli kwa maisha yao wenyewe. Mtu yuko radhi kufanya kitu ambacho hakipendi na hakimlipi kwa sababu tu hataki kujitesa zaidi.

Lazima uwe mkweli kwako mwenyewe kama unataka kupiga hatua zaidi.

Usipokuwa mkweli kwako mwenyewe utaishia kutafuta kila aina ya sababu.

Bila kuishi kwenye ukweli, hutapiga hatua bali utaishia kubaki pale pale.

Usijidanganye, ishi maisha ya uhalisia wako. Fanya kile ambacho ni sahihi kwako. Kama maisha ni magumu pambana kuhakikisha unayavuka hayo magumu.

Tumekuwa na kauli moja ya kujiambia, tushukuru kwa kila jambo, hata una maisha magumu unashukuru?

Kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako halafu unashindwa kukikamilisha huo ni uzembe hupaswi kushukuru. Kila siku unachelewa kwenye kufungua biashara au kufika kazini halafu unashukuru wakati kuwahi iko ndani ya uwezo wako.

Kwa nini uishi kwenye uhaba wakati asili ina utele?

Usiendelee kutafuta sababu kwa sababu sababu hazilipi bili. Inabidi ufikie mahali ukiona kitu unachofanya hakikulipi jilipue ukafanye kile kinachokulipa.

Wewe siyo mti au mbuzi aliyefungwa kamba kiasi kwamba huwezi kujiongeza. Jifungue kamba na nenda katafute majani mazuri sehemu yaliko.

Hatua ya kuchukua leo; Pambana kupata maisha bora kuliko kuvumilia maisha magumu.

Kwahiyo, kama maisha ni magumu jua wewe ndiyo unayafanya kuwa magumu zaidi kwa sababu ya kutokuchukua kwako hatua.

Uamuzi ni wako kuendelea kuvumilia maisha magumu au kupambana kupata maisha bora.
Kazi ni kwako, mimi nimechagua kupambana kupata maisha bora na siyo kuvumilia maisha magumu.
Hujaja duniani kuvumilia maisha magumu bali kufurahia maisha mazuri na hayo yote wewe ndiyo mwenye kibali cha kuamua kuishi maisha magumu ya kuvumilia shida au kupambana kupata maisha bora.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: