Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kinachoendelea Ndani Yako Kinaonekana Kwa Nje

Mwandishi Earl Nightingale aliwahi kunukuliwa akisema, kinachoendelea ndani yako kinaonekana kwa nje.

Kile unachofikiri kinaamua ni nini utafanya. Kila unachofikiri kila mara kitaamua ni wapi utakapoishia na maisha yako.

Hapo wala hakuna ubishi. Mawazo yako unayowaza yawe ni chanya au hasi ndiyo yanakufanya wewe uonekane hivyo ulivyo.

Ukifikiria mawazo ya kujenga, utaona matokeo mazuri unayotaka kuyaona yanakuja.

Kila siku shirikiana na watu wenye mawazo ya mafanikio.

Tengeneza timu ambayo mtashirikiana na kusaidiana, kwa kufanya hivyo utajitengenezea uhakika wa kufanikiwa.

Hatua ya kuchukua leo; fikiria mawazo ya kujenga mara zote.

Kuwa na fikra za kujenga kwani hizo ndiyo zinazalisha matendo ya kujenga na kukuwezesha kufanikiwa zaidi.

Kumbuka, kinachoendelea ndani yako kinaonekana kwa nje, je, nini kinaendelea ndani yako?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: