Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tafuta Mtu Wa Kukuwajibisha

Kwa sababu sisi binadamu ni wavivu kiasili. Usipokuwa na mtu anayekuwajibisha ni vigumu kuchukua hatua.

Kama unaona nidhamu binafsi bado ni tatizo tafuta mtu ambaye atakuwajibisha yaani accountability partner. Mtu ambaye unamweshimu na wala hutoweza kumwangusha hata kidogo.

Wakati mwingine unaweza kumpa kiasi fulani cha fedha kwamba akae na hizo fedha usipofanya kitu fulani basi azichukue. Hii itakuuma na itakusukuma kujituma.

Nidhamu binafsi ya kujisimamia ni tatizo kwa wengi. Mtu anapanga kila siku na anajua nini anatakiwa kufanya lakini hana nidhamu ya kuchukua hatua. Mwingine asipokuwa na mtu anayemsukuma anaona ni fanye au nisifanye hakuna mtu atakayeniambia chochote kile.

Kama kila mtu akiwa na mtu wa kumwajibisha basi watu wengi wangefanya makubwa sana.

Uwe makini sana na uvivu, uzembe na ujinga ni vitu vya kawaida sana lakini vinachangia kufanya maisha yako yarudi nyuma na siyo kwenda mbele.

Usiogope kulipa gharama itakusaidia sana. Watu huwa wanakuwa wanajisukuma kwenye vitu ambavyo wanalipia. Vitu ambavyo watu hawalipii huwa hawajisumbui hata kuvithamini.

Unayo bahati sana katika maisha yako. Hivyo unachotakiwa kufanya ni kuandaa mazingira ya kukutana na bahati hiyo.

Hatua ya kuchukua leo; ifikie mahali ujitoe mwenyewe bila kujisukuma. Jichangamotishe mwenyewe je, kwa mwenendo unao kwenda nao utafika kweli?

Ukitaka ufanye makubwa ambayo hujawahi kufanya kwenye maisha yako, tafuta mtu wa KUKUWAJIBISHA. Kwa sababu sisi binadamu ni wavivu kiasili, usipokuwa na mtu wa kukusumbua unakuwa mzembe.
Ukweli ni kwamba yako mambo mengi unashindwa kutekeleza kwa sababu ya uvivu kwa nini sasa usitafute mtu anayekusukuma kuchukua hatua na ambaye yeye anahitaji matokeo tu na siyo sababu.

Rafiki yangu, Mimi niko kwa ajili yako, ukiwa unahitaji mtu wa kukusukuma kwenye mkwamo wowote karibu sana.

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: