Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tulia Kwenye Eneo Hili

Kama unataka kufikia kitu fulani kwenye maisha yako, iwe ni ndoto au lengo kubwa au kitu chochote kile unapaswa kutulia kwenye eneo la mchakato.

Tulia kwenye mchakato na mafanikio yatakuja yenyewe.

Kumbuka kuwa mchakato ndiyo zawadi. Ndiyo lengo la kufanya. Unafanya ili ufike kule unakotaka kufika.

Mchakato ni kama mwendesha baiskeli, ili afike anapaswa kuendelea kupiga pedeli ili baiskeli iendelee kuwepo katika mwendo. Mchakato ndiyo njia ya kukusaidia wewe kufika kule unakotaka kwenda.

Mchakato ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu sisi. Tunaweza kuathiri lakini matokeo ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wetu sisi. Hatuwezi kuathiri matokeo lakini tunaweza kuathiri mchakato.

Kazi yako iwe ni kufanya kazi yako halafu matokeo tuiachie asili ifanye kazi yake.

Wewe hakikisha unatimiza wajibu wako ambao ndiyo mchakato wa kupata kile unachotaka na kisha matokeo yetu yataamuliwa na mchakato wetu.

Kadiri tunavyokuwa kwenye mchakato ndivyo tunavyopata zawadi nzuri. Mchakato ni zawadi ambayo tunaipata kwenye matokeo.

Watu wengi wanaliogopa eneo la mchakato na kulipenda eneo la matokeo. Hakuna matokeo bila mchakato. Kazi iko kwenye mchakato na siyo kwenye matokeo.

Jiulize unataka nini, kisha kimbilia kwenye mchakato haraka wa kule unakotaka kwenda.
Usijiulize utafanya nini badala yake fanya kile unachopaswa kufanya kadiri ya lengo lako.

Hatua ya kuchukua leo; usiache kufanya mchakato wa kile unachotaka kwenye maisha yako kwa sababu ndiyo zawadi yako.

Ukiacha kufanya mchakato, huwezi kufika kule unakotaka kwenda. Mchakato ndiyo kazi yenyewe na iko ndani ya uwezo wetu tunaweza kuiathiri kwa namna yoyote ile.
Usihangaike na matokeo bali hangaika na mchakato maana ukifanya vizuri sana kwenye mchakato na matokeo yatakuwa mazuri sana

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: