Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Watoto ni matunda ya ndoa.
Watoto wenye maadili mazuri huwa wanatokea familia zenye maadili mazuri. Watoto wanakua bora pale ambapo wazazi wanakuwa bora.
Shabaha yetu kubwa ya leo ni mzazi au mlezi kuepuka kuwalinganisha watoto.
Usiwalinganishe watoto wako kwa sababu utakosa kujua upekee wao.
Watoto huwa hawafanani hata siku moja. Kila mtoto ana upekee wake ambao watoto wengine hawana.
Mzazi au mlezi unapaswa kuwapokea watoto kama walivyo. Mtumie kila mtoto kadiri ya upekee wake.
Epuka kuwalinganisha watoto wako kwa uwezo wa kidarasani. Hii itawafanya watoto wajigawe na kuleta mpasuko katika familia.
Wewe kama mzazi kuwa mzazi wa wote awe anafanya vizuri au hafanyi vizuri wewe ndiyo uwe mtu wake wa kwanza wa kumtia moyo.
Usiwatamkie watoto maneno hasi ambayo yatawakatisha tamaa. Kila mtoto ana upekee wake hivyo tumia huo upekee wake kumfanya awe bora kwenye kile anachofanya.
Ukiwachukulia watoto kama vile walivyo utaweza kuwalea vizuri sana. Lakini ukiwagawa kwa kuwalinganisha utakosa upekee wa watoto ulionao.
Hatua ya kuchukua leo; wapokee watoto kama walivyo na usiwalinganishe watoto kadiri ya udhaifu na uimara walio nao.
Kwahiyo, wapatie watoto malezi bora ambayo hawatakuja kuyapata sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa kwako.
Kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako; kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Ni haki ya mtoto kupewa malezi bora kutoka kwa mzazi au mlezi.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo