Sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Na karibu kila mmoja wetu ana husiana na wengine.
Kitu kimoja kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka kutoka kwa wengine ni mawasiliano mazuri. Hakuna kitu ambacho unaweza kukipata bila kuwa na mawasiliano na wengine.
Mawasiliano ndiyo kiunganishi muhimu kinachotuwezesha sisi kupata kile tunachotaka. Chochote unachotaka kutoka kwa wengine utakipata kwa njia ya mawasiliano.
Unaweza ukawa na kila kitu lakini ukiwa na mawasiliano mabaya na wengine ni ngumu kwako kupata kile unachotaka kutoka kwa wengine.
Jifunze namna ya kuwasiliana vizuri na watu. Jua saikolojia za watu na watumie vizuri watu kupata kile unachotaka.
Kuwa na mawasiliano mazuri ambayo yana ushawishi ya kuvuta kile unachotaka. Mawasiliano mazuri kwako ni kama sumaku, utaweza kuvuta kile unachotaka kutoka kwa wengine.
Pale unapoianza siku yako jipange kuwa na mawasiliano mazuri na wengine. Usipokuwa na mawasiliano mazuri na wengine ni wazi kwamba huwezi kushinda kile unachotaka. Watu wako tayari kukupa kile unachotaka kama umeweza kuwasiliana nao vizuri.
Wako watu ambao wanakosa kile wanachotaka kwa sababu ya kuwa na mawasiliano mabavu. Usiwe mtu wa aina hiyo, kuwa mtu ambaye ana mawasiliano mazuri na wengine ili uweze kupata kile unachotaka.
Hatua ya kuchukua leo; Kawasiliane vizuri na wengine.
Kuwa na lugha yenye ushawishi kwa wengine kiasi kwamba wengine wawe tayari kukubaliana na wewe.
Ukikosea kwenye mawasiliano utakosea kila mahali na watu watakunyima kile unachotaka kutoka kwao.
Mawasiliano mazuri ni silaha ya kupata kile unachotaka kutoka kwa wengine. Kawe na mawasiliano mazuri na wengine ambayo yatakusaidia wewe kushinda na wengine kushinda. Kuwa na mawasiliano ya kila mmoja kushinda na siyo wewe kushinda na wengine kushindwa.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo
Habari Kessy,
Asante sana kwa makala ya umuhimu wa mawasiliano katika mafanikio makubwa tunayotaka.
Ninashukuru sana.
LikeLike
Salama Mr Aliko, Asante sana.
LikeLiked by 1 person