Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Matatu Ya Kuepuka Kuyaanika Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Unaruhusiwa kuanika vitu vyote lakini siyo hivi vitatu ninavyokwenda kukuambia leo.

Moja ni hali yako ya afya. Watu hawapaswi kujua juu ya hali yako ya kiafya. Kwa sababu watu wakishajua uimara au udhaifu wako wa kiafya wataweza kutumia mtego huo kupata kile wanachotaka kutoka kwako. Masula ya afya yako binafsi ni siri na wala siyo suala la kuanika kwenye mitandao ya kijamii. Watu wasiokuwa na mapenzi mema wataweza kutumia vibaya taarifa zako na kisha kukuumiza.

Mbili ni hali yako ya kifedha. Siyo kila mtu atapenda kuona unafanikiwa. Hata kama una fedha nyingi hutakiwi kuwaonesha watu kuwa una fedha maana hii inachangia kuleta shida baadaye. Watu wakigundua una fedha ni rahisi kukaribisha matatizo. Lakini pia, inaibua wivu ambao hata haukupaswa kuwepo.

Hali yako ya kimahusiano ya kifamilia. Siyo jambo zuri kuanika mambo yako ya kifamilia kwenye mitandao ya kijamii. Watu wasiokuwa na mapenzi mema na wewe wanaweza kutumia taarifa zako za kifamilia kukufanyia kitu ambacho siyo kizuri kwako.

Vitu hivi vitatu huwa vinaibua hisia na kupelekea hata watu kutapeliwa na kuumizwa vibaya.

Hatua ya kuchukua leo; tafadhali naomba usianike mambo yako ya kifamilia, hali yako ya afya na fedha ulizonazo kwenye mitandao ya kijamii.

Vitu hivi vitatu viwe ni siri yako na siyo kuanika kila mtu ajue Watu wakishajua mambo yako binafsi watatumia kukulaghai na kukutumia kuumiza au kutumia hiko kama chanzo cha kukutaka uwape kile wanachotaka kutoka kwako.

Umepewa uhuru lakini usitumie uhuru wa kwenye mitandao ya kijamii kuanika kila kitu kuhusu wewe. Anika yote lakini usianike hali yako ya afya, familia na fedha ulizonazo. Kuwa makini kile unachoanika kwa wengine.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: