Ukiwa unataka kwenda sehemu fulani huwezi kusema utaanzia wapi? Kwa mfano, uko nyumbani na unataka kwenda kazini huwezi kujiuliza hivi utaanzia wapi ili ufike eneo la kazi bali utaanzia hapo hapo nyumbani kutoka na hatimaye utafika kazini.
Vile vile katika safari ya kuanza kutengeneza utajiri unaianzia hapo hapo ulipo. Anza na kile ulichonacho badala ya kusibiri kile usichonacho.
Safari inakua rahisi kama ukianzia hapo ulipo kuliko kutamani kufika safari bila ya kuanza.
Unaweza ukaanza maana kuanza ndiyo mtihani mkubwa kwa watu wengi. Ukianzia hapo ulipo utakua ni kama vile umeondoa laana.
Kama ulikuwa unajiuliza je, utaanzia wapi sasa umeshapata jibu lake, anzia hapo ulipo. Anza na kile unachofanya, ulichonacho na utafika kule unakotaka kufika.
Hatua ya kuchukua leo; Kuwa na fikra za kitajiri za kufikiri katika uchanya na siyo uhasi. Amini kuwa mambo yanawezekana kama ukianzia hapo hapo ulipo.
Usidharau pale ulipo na wala usidharau kile ulichonacho. Sehemu ambayo utaweza kuanzia kutengeneza utajiri ni hapo ulipo sasa.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo
Asante sana kwa makala nzuri,
Mimi,
Aliko Musa
LikeLike
Karibu sana Mr Aliko Musa
LikeLiked by 1 person