Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Limepangwa Kutokea Litatokea Tu

Kwa sababu mambo mengi yanayotokea yako nje ya uwezo wako. Huwezi kuzuia baridi au jua lisitoke. Huwezi kuzuia mtu asife kwani vitu vingine viko nje ya uwezo wako huwezi kuvidhibiti kamwe.

Watu wengine wanajikuta wao ndiyo viranja wa dunia. Wanataka mambo yaende kama vile wanavyotaka wao. Huwezi kudhibiti tukio fulani lisitokee.

Kama limepangwa kutokea litatokea tu. Huwezi kuizuia asili kutenda kile ambacho asili imepanga.

Uwe unapitia mazuri au mabaya yote shukuru kwa sababu huwezi kujua makusudi ya asili. Kwa nini asili imeruhusu jambo fulani kutokea.

Kile ambacho unaweza kukidhibiti fanya hivyo. Kile ambacho huwezi kipo nje ya uwezo wako achana nayo kisikusumbue. Ukipambana na dunia, hutaiweza.

Hatua ya kuchukua leo; Fanya yale ambayo yako ndani ya uwezo wako. Yale ambayo yako nje ya uwezo wako iachie asili ipambane nayo.

Kwa hiyo, asili ikiamua kufanya kile inachotaka inafanya wala huwezi kuizuia.
Huna nguvu ya kuzuia matukio ya dunia yasitokee. Asili siku huwa haina baya wala zuri.
Ukiishi katika mtazamo huo wa kifalsafa utaona yote yanayotokea hayajakuonea.

Kumbuka, asili ina upacha kwenye kila jambo. Na kila jambo lipo kwa ajili yetu. Kama ni mazuri basi jua kuna mabaya pia ambayo yanatuhusu wote.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: