Ubize ni neno ambalo linaongelewa karibu na kila mtu. Ukikutana na mtu utamsikia akisema niko bize aisee. Je, umeshawahi kukaa chini na kuhoji ubize wako?
Kila siku uko bize, lini utakua huru? Je, ubize wako ni ubize hasi au chanya? Wengi wako bize je, huo ubize wao matokeo yake yanaonekana? Au ubize jina tu?
Ubize usiokuwa na matokeo huo ni ubize hasara. Ukichunguza watu wengine wako bize kweli lakini siyo kwenye uzalishaji bali ni ubize bora siku ziende.
Kama uko bize kweli na kufanya kazi mbona hatuoni matokeo mazuri? Kazi huwa haidanganyi kama ukiweka kazi lazima matokeo yaonekane. Kama wewe uko bize na kazi mbona maisha yako hayabadiliki? Ukiangalia mwaka jana na mwaka huu yako vile vile. Huoni huo ni ujinga? Kuwa vile vile kila siku huku ukitegemea kupata matokeo mazuri?
Watu wengi hawako bize katika uzalishaji bali wanajificha katika mwamvuli wa ubize ili nao waonekane wanafanya kazi.
Wengi wanatoroka majukumu yao huku wakisingizia niko bize. Niko bize kimekuwa ni kichaka kwa watu wengi kuficha udhaifu wao na kutowajibika ipasavyo.
Uko katika familia lakini unasema uko bize unakosa hata muda wa kukaa na familia yako. Hivi umeshawahi kujiuliza gharama ya kuharibu familia? Familia ikiharibika utafurahia na na nani mafanikio unayotafuta?
Uwe mtu wa kulinda kile unachojenga. Linda kile unachowekeza kwa maana ulitumia gharama hivyo usiache nguvu zako zipotee bure.
Kama huwezi kulinda kile unachojenga ni bora usifanye. Kokote ulipowekeza, linda uwekezaji wako. Hakikisha macho yako, yapo pale ambapo fedha yako umewekeza.
Hatua ya kuchukua leo; Pima ubize wako. Chunguza ubize wako una maana?
Kama unakuingizia fedha basi vizuri sana lakini kama unakuingizia hasara pole sana acha mara moja.
Usitumie ubize kama kichaka cha wewe kushindwa kufanya majukumu yako ya msingi. Wako ambao wanapoteza sifa zao kwa sababu tu ya kusema niko bize. Niko bize siyo mtu mzuri kwani anasababisha watu kushindwa kuchukua hatua katika wajibu wao.
Timiza wajibu wako, niko bize hana faida kwako. Maisha ni yako, usimsingizie niko bize.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo