Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Cha Uhakika Kupata Pale Unapothubutu Kufanya Jambo Lolote Lile

Ni changamoto.

Niambie ni jambo gani ambalo utasema ulianze halafu usikutane na changamoto njiani? Kila kitu kina changamoto ndiyo maana huwa nashangaa mtu anayeacha kufanya jambo lake kwa sababu ya changamoto.

Ukiingia kwenye biashara kuna changamoto zake na changamoto ni kitu cha uhakika kuliko hata faida.

Ukiwa kwenye ajira nako pia kuna changamoto zake. Kifupi hakuna sehemu salama ambayo utasema hapa hamna matatizo. Kama kuna sehemu ambayo haina changamoto hapa duniani naomba unishirikishe uzoefu wako.

Ukiwa katika maisha ya wito wowote ule kuna changamoto yake. Kikubwa ni kubeba misalaba tuliyopewa huku tukimtegemea Mungu maana bila Mungu misalaba tuliyonayo hatuwezi kuibeba bila msaada wa Mungu. Kibinadamu kuna mahali tunachoka na kufikia ukomo lakini tukiibeba kwa msaada wa Mungu misalaba yetu inakuwa si misalaba migumu.

Asili inamtaka kila mmoja wetu kupata kitu katika hali ngumu ili aweze kujifunza na kuona thamani ya kitu. Vipi kama tungekuwa tunavipata vitu kirahisi tungevithamini? Tunapata muda bure lakini ni wangapi wana thamini muda?
Nafasi ya kuwa hai na kuvuta pumzi ni bure lakini ni wangapi wakiwa hai na wazima wanashukuru hata kwa nafasi hiyo?

Jiwekee akilini kuwa hakuna kitu ambacho hakina changamoto. Kwa kulitambua hilo ukikutana na changamoto isiwe ndiyo mwisho wa kuendelea bali uwe mwanzo wa kuendelea na kile ulichoanzisha.

Ukithubutu kufanya jambo lolote lile, jiandae kukutana na changamoto. Changamoto ni shule ya maisha itakayokupitisha kuvuka darasa moja kwenda lingine.

Hatua ya kuchukua leo; Usidanganyike, kila kitu kinachangamoto yake. Unapoamua kuchagua kitu cha kufanya basi usiangalie faida tu bali fanya kile kitu kwa sababu unakipenda.

Bila kupenda kile unachofanya utajikuta ni mtu wa kuona changamoto za kila aina. Utaona kila kitu ni mzigo kwako lakini ukipenda kitu hutaona changamoto kama ni kikwazo kwako kufika kule unakotaka kufika.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: