Design a site like this with WordPress.com
Get started

Namna Bora Ya Kurudisha Neno Ulilozungumza

Unapozungumza unapaswa kuwa makini kwa sababu neno unaloongea ni kama vile unarusha jiwe gizani na hujui nani litampata.

Ukishaongea, umeaongea na watu watatafsiri vile wanavyojua wao kadiri ya hisia walizokuwa nazo.

Kifupi, namna bora ya kurudisha neno ulilozungumza ni kutolisema tu.

Kuwa mwangalifu na maneno yako, kumbuka hakuna namna nyingine ya kulirudisha neno ulilozungumza isipokuwa kutokulisema kabisa.

Tawala mdomo wako. Matatizo mengi yanaibuliwa na mdomo. Ndiyo maana huwezi kumkuta bubu amegombana na mtu kisa ya mdomo.

Wanafalsafa wanatushauri kuwa ongea pale ambapo ni muhimu tu. Yaani usipoongea mambo yatakuwa hayaendi.

Jifunze namna ya kutumia maneno yako vizuri sana. Wako watu ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii kwa sababu wanajua namna ya kupanga maneno.

Kwa mfano, Mwl. Nyerere alitoa maneno yenye ushawishi sana wakati wa vita vya kagera. Yale maneno yalikuwa hivi ” sababu ya kumpiga tunayo, uwezo wa kumpiga tunao, nia ya kumpiga tunayo.” Haya maneno yalikuwa na hamasa kwa wapiganaji.

Kumbe basi, maneno yanaweza kujenga au kubomoa. Ukitamkiwa maneno mazuri kila siku yatakuathiri katika namna chanya na kinyume chake yatakupa athari hasi.

Tumia maneno yako vizuri kuunganisha watu na siyo kutenganisha mahusiano ya watu.

Na kuna watu wanakosana na watu kwa sababu ya kutumia maneno vibaya. Usitumie maneno yako vibaya bali yatumie vizuri ili uweze kupata ushindi unaotaka.

Hatua ya kuchukua leo; Fikiri kwanza kabla ya kuongea. Ukiwa na hisia jicheleweshe kuongea.
Ongea pale ambapo ni muhimu kuongea na kama siyo lazima kuongea usiongee kwani kukaa kimya siyo ujinga ni ujanja maana utajiepusha na mengi.

Maneno ni kama dawa tamu, Ukitumia vizuri itakusaidia na ukitumia kwa fujo na kuinywa sana kwa sababu ni tamu itakuharibu.
Kuwa makini na maneno yako unayoongea.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: