Huwa ninashangaa sana pale ambapo mtu anakuwa anamiliki kitu kizuri ambacho ametumia gharama kukitengeneza lakini cha ajabu hana hata mpango wa masoko au mauzo.
Unapozalisha kitu ili watu wengine wakipate andaa mpango wa masoko. Unaweza ukawa na bidhaa bora lakini kama watu hawaijui ni sawa na bure. Bidhaa ikishazalishwa ipeleke sokoni. Na wale ambao ni wahitaji wajue kile unachouza.
Kujitangaza kwa walengwa ndiyo masoko yenyewe. Watu wana mambo mengi bila kuwaambia unauza bidhaa fulani na inakwenda kusaidia kutatua changamoto inayowakabili lazima watachukua hatua.
Wako watu wameandika vitabu lakini hawavitangazi. Bila kuwaambia watu una nini hawezi kujua. Kama unafanya kitu halafu unashindwa kukipeleka sokoni ni bora usikifanye. Lengo la kufanya kitu ni watu wasaidike na kile ulichofanya sasa tumia nguvu kuwajulisha walengwa wako kuwa una kitu fulani na mtu anapohitaji anajua atapata wapi.
Hakikisha watu wanajua kupitia wewe watu wanaweza kufaidika na nini. Usikae na kile unachojua. Kama unajua kuimba wasaidie wengine kuimba kwani asili ya dunia inataka kuwawezesha wengine. Usipotoa utanuka na kuonekana huna faida.
Hivi hujiulizi kwa nini mitandao ya simu kila siku inatangaza bidhaa zake? Watu ni wagumu kuchukua hatua hivyo kujirudia rudia kwa tangazo la bidhaa fulani inamsaidia kuelewa na kuchukua hatua.
Chochote kile unachouza, hakikisha unakuwa na mpango wa mauzo na masoko. Kwenye masoko na mauzo ndiyo mahali fedha ilipo. Kama huwezi kuweka juhudi kwenye masoko na mauzo ni bora usijisumbue kuzalisha chochote kile unachofanya.
Hatua ya kuchukua leo; Acha watu wajue unauza nini, acha watu wajue kupitia wewe watanufaika na nini.
Acha watu wajue unafanya nini.
Dhihirisha kwa walengwa kile ambacho unacho. Zalisha, kisha peleka mahali sahihi.
Kuwa na timu ya masoko na mauzo. Kuwa na watu makini wanaojua nini unataka. Mteja akitaka bidhaa basi unamsaidia haraka.
Kila kitu ni biashara. Usifanye chochote kwa kubahatisha, fanya kile unachofanya kama kazi na siyo “hobi”.
Usiingie kwenye biashara yoyote kama hauko tayari kuwahudumia wateja wako kile wanachotaka. Ukisema unauza chakula, basi watu wakija kutaka chakula wakipate na siyo sababu. Fanya kazi kwa ubora, maisha yako ni biashara je yanauzika?
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo